Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, October 9, 2013

Ikhwan yaondolewa katika orodha ya NGO Misri


Ikhwan yaondolewa katika orodha ya NGO Misri
Harakati ya Ikhwanul Muslimin sasa imefutwa kikamilifu nchini Misri baada ya serikali kuamuru kundi hilo liondolewe katika orodha ya mashirika yasiyo ya kiserikali NGO nchini humo.  Uamuzi huo wa serikali ya Misri wa kuiondoa Ikhwanul Muslimin katika orodha ya NGO umechukuliwa siku kadhaa baada ya kundi hilo la kisiasa kupigwa marufuku.
Baada ya kuingia madarakani serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi nchini Misri zimechukuliwa hatua kali dhidi ya harakati ya Ikhwan hasa baada ya kupinduliwa rais wa zamani wa nchi hiyo aliyechaguliwa na wananchi Muhammad Musri mwezi Julai. Wengi wanaamini kuwa uamuzi huo sasa unaandaa mazingira ya jeshi la Misri kuwatia mbarozi zaidi wafuasi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.