Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, October 8, 2013

Makanisa ya Kenya yajitosa kwenye mgogoro wa ICC


Makanisa ya Kenya yajitosa kwenye mgogoro wa ICCViongozi wa makanisa nchini Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutoshirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake mjini Hague, Uholanzi.
Wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa la AIPCK,  Mugecha Karume, viongozi hao wa makanisa  wamesema kuwa, kesi hiyo ina  mambo mengi yasiyoeleweka na kwa mantiki hiyo, hakuna haja Rais Kenyatta kwenda Hague kwa ajili ya kesi dhidi yake mbele ya mahakama hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na mtangazaji wa radio Joshua Sang wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya Wakenya 1000 waliuawa. Kwa sasa Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na Joshua Sang wako mjini Hague ambako kesi zao zinaendelea. Kesi ya Rais Kenyatta inatarajiwa kunza mwezi ujao wa Novemba. Umoja wa Afrika AU pia umetaka kesi hizo zisimamishwe au kuhamishiwa jijini Nairobi ili zisikizwe na mahakama za Kenya.