Makundi makuu ya upinzani nchini Bahrain yamesusia mazungumzo ya
maridhiano ya kitaifa katika kulalamikia ukandamizaji wa utawala wa nchi
hiyo. Jamil Kazem msemaji wa makundi hayo yanayoongozwa na harakati ya
al Wefaq amesema kuwa, wameamua kususia mazungumzo hayo kutokana na
kukosekana mageuzi ya kweli na ukandamizaji wa watawala wa Bahrain.
Utawala wa Aali Khalifa ulianzisha mazungumzo hayo ya kitaifa kama
sehemu ya jitihada za kutuliza upinzani na kuhitimisha mwamko wa
wananchi wa kutaka mageuzi.
Hayo yanajiri huku korti moja ya nchi hiyo Jumapili ikiwahukumu raia 50 wa madhehebu ya Shia kifungo cha miaka 15 jela, kutokana na kuunda kundi la upinzani linalojulikana kama 'Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14.' Amnesty International na makundi mengine ya kutetea haki za binadamu yamelaani hukumu hiyo.