Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema mwishoni mwa wiki, kuwa serikali ya Uingereza haipaswi kufuata nchi zingine za ulaya kwa kupiga marufuku vazi la Niqabu. Hata hivyo amesema taasisi kama shule mahakama waruhusiwe kuweka kanuni zao wenyewe.
Suala la wanawake wa kiislamu kuvaa Niqabu ni ajenda inayotawala kwa sasa nchini Uingereza baada ya Jaji mmoja alipogoma kumruhusu mwanamke kutoa ushahidi mahakamani kwa kuwa amevaa Niqabu na chuo kilichopiga marufuku vazi la Niqabu kitu kilichopelekea upinzani na maandamano kutoka kwa jamii ya kiislamu.
"Sisi ni nchi huru na watu wanapaswa kuwa huru kuvaa
chochote wanachopenda katika jamii au binafsi", aliiambia Televisheni ya BBC siku ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa chama cha Conservative huko mji wa Manchester.

"Lakini sisi tunapaswa kusaidia taasisi juu ya haja ya kuweka sheria ili waweze kufanya kazi vizuri.
Na katika mahakama wawe na utaratibu maalumu wa kuona sura ya mtu", alisema Waziri Mkuu huyo wa Uingereza.
inayokadiriwa kufikia watu milioni 2.7, bila ya kuzuia haki ya uhuru wa kuabudu. Ufaransa na Ubelgiji zimepiga marufuku uvaaji wa Niqabu maeneo ya Umma.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron |
No comments:
Post a Comment