Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, October 2, 2013

US gizani, mshahara wa Obama wasimamishwa


US gizani, mshahara wa Obama wasimamishwa
Ikulu ya Marekani White House imetoa amri ya kufungwa baadhi ya mashirika ya serikali ya shirikisho baada ya Bunge la nchi hiyo kushindwa kupasisha bajeti ya kuzuia kusimaishwa shughuli za serikali.
Amri hiyo ya kufungwa baadhi ya taasisi za serikali ya Marekani ilitolewa jana dakika kumi kabla ya serikali kuishiwa rasmi na fedha za matumizi.
Kutokana na hali hiyo wafanyakazi yapata milioni moja wa serikali wanapewa likizo ya lazima bila ya malipo. Vilevile thuluthi mbili ya wafanyakazi wa serikali akiwemo Rais Barack Obama, watalazimika kufanya kazi bila ya malipo hadi mgogoro wa bajeti kati ya Warepublican na Wademokrat utakapotatuliwa. Kufungwa kwa mashirika ya serikali ya shirikisho pia kutapelekea kufungwa mabustani ya taifa na kukwamisha miradi ya utafiti wa tiba.
Wademokrat na Warepublican wanazozana juu ya miswada iliyopendekezwa na serikali ya Obama juu ya marekebisho ya bima ya afya.