Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, March 29, 2013

Picha za Muonekano wa Ghorofa lililoanguka Asubuhi ya Leo Kariakoo












Mabaki ya jengo hilo lililoporomoka jijini da es salaam amablo lipo barabara ya morogoro mtaa wa indiana.Huku ni mashuhuda watukio hilo wakiwa eneo hilo muda huu..Maiti zaidi zinaokolewa bado idadi kamili haijafahamika mpaka sasa.Endelea kupitia audifacejackson blogspot kwa taarifa ziadi

Monday, March 25, 2013

Uamsho haina account wala page facebook



Masoud Khamis Al-Bimani

Jumuia ya UAMSHO na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar haina account wala page ya Facebook, lakini kuna watu kwa makusudi wameamua kutengeneza Page ya Uamsho hapa FB, kwa lengo la kuitia Doa jumuiya, anakua anapost vitu visivyo na Maana, kwa lengo la kuupotosha Umma tujihadhari na watu hawa.

Kesi ya Uamsho yasomwa upya, yapangiwa Jaji Fatma



KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na
Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) imeanza kusomwa upya leo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar baada ya maamuzi ya awali kutenguliwa.

Kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid
Mahmoud na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ramadhan Nassib, ambae
aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni,

Wednesday, March 20, 2013

Rwanda yawanyima viza wataalamu wa UN


Rwanda yawanyima viza wataalamu wa UN
Rwanda imekataa kutoa viza kwa maafisa wawili wa timu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliyoituhumu Kigali mwaka jana kuwa inawapa silaha waasi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuwataja kuwa watu wenye upendeleo.

Al Qaeda wamuua mateka wa Kifaransa


Al Qaeda wamuua mateka wa Kifaransa
Mtandao wa al Qaeda wa kaskazini mwa Afrika umetangaza kuwa umemuua mateka wa Kifaransa katika kulipiza kisasi uingiliaji wa kijeshi wa Ufaransa nchini Mali. Mateka huyo wa Kifaransa kwa jina la Phillippe Verdon alikatwa kichwa na mtandao huo wa al Qaida tarehe kumi mwezi huu katika kile kundi hilo lilichokisema kuwa ni kulipiza kisasi cha mashambulizi yaliyoanzishwa na Paris huko Mali. Verdon alikuwa mmoja kati ya raia wawili wa Ufaransa waliotekwa nyara mwezi Novemba mwaka juzi huko kaskazini mwa Mali katika mji wa Hombori. 

Polisi ya Misri yamtia mbaroni binamu wa Gaddafi


Polisi ya Misri yamtia mbaroni binamu wa Gaddafi
Polisi ya Misri imesema kuwa imemtia mbaroni binamu na aliyekuwa mpambe wa karibu wa Muammar Gaddafi kiongozi wa zamani wa Libya. Hapo jana maafisa wa Misri walisema kuwa Ahmed Gaddaf al Dam alitiwa nguvuni baada ya vikosi vya usalama kuizingira nyumba yake katika kitongoji cha Zamalek huko Cairo. Afisa mmoja wa Misri amesema kuwa afisa huyo wa zamani wa intelijinsia wa utawala wa Gaddafi atakabidhiwa kwa maafisa wa Libya hivi karibuni. Baada ya kuzingirwa nyumba yake kwa masaa kadhaa huko katikati mwa Cairo, binamu huyo wa Muammar Gaddafi alisikika akizungumza na kanali moja ya televisheni kwa njia ya simu na hapa ninamnukuu" tulifika hapa kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na baraza la kijeshi, sisi si magaidi wa kuweza kushambuliwa namna hii," mwisho wa kumnukuu.  

Tuesday, March 19, 2013

37 wafariki dunia katika ajali ya basi India


37 wafariki dunia katika ajali ya basi IndiaPolisi ya India imetangaza kuwa kwa akali watu 37 wamepoteza maisha na wengine 17  kujeruhiwa, baada ya basi la abiria walilopanda kupoteza mwelekeo na kutumbukia katika  mto wa Jagbudi magharibi mwa nchi hiyo.
Polisi ya India imeeleza kuwa, ajali hiyo mbaya imetokea mapema leo alfajiri katika wilaya ya Maharashtra. Polisi ya Usalama barabarani nchini India imeeleza kuwa, basi hilo lilikuwa likitokea katika mji wa Goa na kuelekea Mumbai; na kwamba  dereva wa basi hilo alishindwa kulidhibiti na kutumbukia mtoni. Polisi imeeleza kuwa, ajali hiyo imetokea umbali wa kilomita 350 kusini mwa Mumbai.
Polisi imeeleza kuwa, watu wasiopungua 17 wamejeruhiwa akiwemo dereva wa basi hilo, ambaye hali yake imeelezwa kuwa ni mahututi. Taarifa za awali zinasema kuwa, ndani ya basi hilo kulikuwa na idadi kadhaa ya watalii kutoka nje ya nchi hiyo.

Siasa za Wamagharibi ni za kindumakuwili


Siasa za  Wamagharibi ni za kindumakuwili
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi ya Bahrain amezikosoa vikali siasa za kindumakuwili za Magharibi kuhusiana na matukio ya kieneo na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Bahrain unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa wa nchi hiyo.
Saeed al Shahabi ameongozana na maelfu ya wapinzani wa Bahrain na kukusanyika mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza mjini London na kusema kuwa, uungaji mkono wa kibubusa wa Marekani na Uingereza kwa utawala wa Aal Khalifa umesababisha utawala huo kuvimba kichwa na kupuuza misingi ya haki za binadamu.
Ameongeza kuwa, siasa za kindumakuwili za nchi za Magharibi sio za kikhlaki na amebainisha kuwa, Washington na London zinapaswa kukomesha uungaji mkono wao kwa utawala wa Bahrain ambao unatenda jinai za mauaji, kuwafunga na kuwashikilia korokoroni wanaharakati na kuwatesa wananchi wa nchi hiyo wanaume na wanawake.

Boko Haram waua walimu watatu Nigeria


Wanamgambo wa Boko Haram wakiwa wamejizatiti kwa silaha NigeriaWalimu watatu wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na watu wenye silaha dhidi ya shule mbili huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Walimu hao waliuawa jana katika mashambulio mawili yaliyotekelezwa na watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kundi la Boko Haram katika mji wa Maiduguri unaopatikana katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Aidha wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika mashambulizi hayo. Kabla ya hapo pia, watu 25 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kutokea milipuko mitano katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria. Hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote lililotangaza kuhusika na mashambulio hayo, lakini kundi la Boko Haram linashukiwa kuwa ndilo lililotekeleza mashambulio hayo kwa vile limekuwa likitekeleza mashambulio kama hayo katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.

Wazimbabwe waipigia kura ya ndio katiba mpya


Wazimbabwe waipigia kura ya ndio katiba mpya
Matokeo yasiyo rasmi ya kura ya maoni ya katiba mpya nchini Zimbabwe, yanaonyesha kwamba, wananchi wameipigia kura ya ndio katiba hiyo ambayo inapunguza madaraka ya rais wa baadaye wa nchi hiyo. Ripoti zilizosambazwa leo kutoka vituo vya kuhesabu kura, zinaonyesha kuwa, watu milioni tatu na laki moja kati ya watu milioni tatu na laki nne waliofika kwenye vituo vya kupigia kura nchini humo, wameipigia kura ya ndio katiba mpya ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inayokabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Gazeti la Herald limeripoti kuwa, watu laki mbili wameipigia kura ya hapana katiba hiyo. Kwa mujibu wa takwimu rasmi za nchi hiyo, Wazimbabwe milioni sita pekee ndio waliokamilisha masharti ya kupiga kura nchini. Ilitarajiwa kuwa, hadi kufikia jioni ya leo, Tume ya Uchaguzi nchini humo ingekuwa imekamilisha kazi za kuhesabu kura na kutangaza matokeo rasmi ya kura hiyo.

Mapigano kati ya jeshi na waasi Sudan Kusini


Waasi wenye silaha nchini Sudan KusiniShirika la Msalaba Mwekundu limetangaza kuwa, zaidi ya watu 60 wamejeruhiwa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi la Sudan Kusini na kundi moja la waasi nchini humo. Shirika hilo limeongeza kuwa, katika kipindi cha wiki mbili zilizopita karibu watu 62 waliojeruhiwa katika apigano hayo walitibiwa katika kituo kimoja cha afya cha shirika hilo na kwamba. Mmoja wa viongozi wandamizi wa shirika hilo amenukuliwa akisema kuwa, idadi rasmi ya maafa yaliyotokana na machafuko hayo ya pande mbili haijafahamika kutokana na kwamba, hadi sasa hakuna taasisi yoyote iliyofika eneo la tukio na kufanya uchunguzi. Ameongeza kuwa, kutokana na viongozi wa Juba kukosa ripoti kamili ya mapigano hayo, idadi ya wahanga inaweza kupindukia ile iliyotajwa hapo awali. Hivi karibuni mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, alielezea kusikitishwa kwake na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na Jeshi la Sudan Kusini dhidi ya waasi wanaoongozwa na David Yauyauambao wanaipinga serikali ya Juba.

Monday, March 18, 2013

Watu 10 wauawa kwenye mlipuko nchini Somalia


Watu 10 wauawa kwenye mlipuko nchini Somalia
Habari kutoka Mogadishu, mji mkuu wa Somalia zinasema kuwa, kwa akali watu 10 wamefariki dunia na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa wa bomu uliotokea karibu na ukumbi wa kitaifa wa michezo ya kuigiza.
Habari zaidi zinasema kuwa, bomu hilo lilikuwa limetegwa kwenye gari na kwamba Mkuu wa Usalama wa Mogadishu ndiye alikuwa mlengwa mkuu. Haijabainika wazi iwapo mkuu huyo ameuawa au la.
Kundi la wanamgambo la Al-shabab tayari limedai kuhusika na shambulio hilo. Kundi hilo limeapa kumuondoa madarakani Rais Hassan Sheikh Mohamud, aliyechaguliwa na bunge la Somalia mwaka uliopita. Hii ni katika hali ambayo, wanamgambo hao wanaripotiwa kuuteka mji wa Hudur wa kusini mwa Somalia.

Wayemen waanza mazungumzo ya kitaifa

Wayemen waanza mazungumzo ya kitaifaYemen imefungua mazugumzo ya maridhiano ya kitaifa yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa ili kuandaa uwanja wa kufanyika uchaguzi na kutungwa katiba mpya kwa shabaha ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu nchini humo.  
Mazungumzo hayo yamefunguliwa na Rais Abdrabuh Mansur Hadi wa nchi hiyo na yanahudhuriwa na zaidi ya wawakilishi 500 kutoka vyama vya kisiasa vya Yemen. Hata hivyo mrengo wa kisiasa wa kusini umesusia mazungumzo hayo na uliitisha maandamano na mgomo katika mji wa Aden hapo jana kupinga suala hilo.

Benki ya Dunia yazisaidia Msumbiji, Malawi na Zambia


Benki ya Dunia yazisaidia Msumbiji, Malawi na ZambiaBenki ya Dunia  kupitia Taasisi ya Maendeleo wa Kimataifa imetoa msaada wa dola milioni 89 kwa serikali za  Msumbiji, Malawi na Zambia kwa lengo la kusaidia  mpango wa chakula salama  na uzalishaji wa kilimo kwenye nchi hizo zilizoko eneo la kusini mwa Afrika.
Hayo yameelezwa na Tijan Sallah Meneja wa Sekta ya Kilimo na Umwagiliaji katika ukanda huo. Sallah ameongeza kuwa lengo la kutekelezwa mpango huo ni kuboresha sekta ya kilimo katika nchi hizo za Kiafrika.  Amesema kuwa, Benki ya Dunia imeamua kutoa misaada yake kwa nchi hizo kwa lengo la kustawisha zaidi utafiti katika sekta ya kilimo na kuboresha mafunzo kwenye sekta hiyo.

Hatari zilizosalia baada ya kukaliwa kwa mabavu Iraq

Hatari zilizosalia baada ya kukaliwa kwa mabavu Iraq Wataalamu wa mashirika ya afya wameripoti kuwa athari zilioachwa huko Iraq baada ya uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya nchi hiyo ni hatari kwa vizazi vijavyo vya nchi hiyo.
Wataalamu wa mambo na mashirika ya afya ya Iraq yametahadharisha kuhusu hatari za athari mbaya za uvamizi na kukaliwa kwa mabavu Iraq na vikosi vya Marekani na kueleza kuwa Marekani ilitumia tani 35 za urani katika vita huko Iraq suala linalotishia maisha ya vizazi vijavyo. Munthi Mahmoud Shukr mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Baghdad ameashiria athari haribifu za urani kwa raia na mazingira ya maeneo yaliyoathiriwa na kueleza kuwa Marekani iliwatumia raia wa Iraq kama mapanya wa maabara na majaribio yake mbalimbali.

Wafungwa wa Guantanamo waendelea kugoma kula


Wafungwa wa Guantanamo waendelea kugoma kula
Mgomo wa kula chakula unaoendelea kufanywa na wafungwa walioko katika jela ya Guantanamo umeingia katika siku ya 41 huku wataalamu wa kitiba na mawakili wanaowatetea wafungwa hao wakionya kuhusu kudhoofika kiafya kwa wafungwa zaidi ya 100 waliogoma kula chakula. Mawakili na maafisa wa tiba wameeleza kuwa wana wasiwasi na hali mbaya ya kiafya ya wafungwa hao walioanza kugoma kula chakula tangu Februari 6 mwaka huu baada ya wafanyakazi wa jela ya Guantanamo kupora vitu vya wafungwa hao zikiwemo barua, picha na nakala za kitabu kitukufu cha Qu'rani wakati walipozikagua seli zao.

Saturday, March 16, 2013

Charity School Bwejuu

Charity School Bwejuu was officially registered with the Ministry of Education and Vocational Training Zanzibar with registration no. PS/225 in 2004. This school has been established under Law no. 6 of 2006, of the Revolutionary Government of Zanzibar.
The school offers compulsory education for orphans and for students coming from poor or dysfunctional families at no cost, but if possible, the families of the students are required to contribute a small amount towards the running cost of the school.





The school welcomes individuals, institutions or government departments to unconditionally support the school in order to achieve our goals. We are grateful to all our sponsors for their financial assistance, which is much needed for providing study materials like books and pens for our students, to finance the running cost of the school and the school's kitchen, pay salaries, upgrade the teachers' educational levels, establish a library and a laboratory, for our hostel and for adding further classes.
The Charity School Bwejuu also receives youth volunteer coaching from all over the world for three months or more. The school provides free lodging for the volunteers on the school grounds.
We welcome individuals and companies to sponsor a student for USD $374 per year or to sponsor a teacher for the school.






CHARITY SCHOOL BWEJUU
P.O. Box 1609,
Zanzibar, Tanzania.
Contact Number: +255777438075
Email: bwejuucharityschool@hotmmail.com
bwejuucharityschool@gmail.com Bank Details:
Account Number: 021- 0000215
Bank Name: Tanzania Postal Bank, Zanzibar Branch
Country:Tanzania
IF YOU NEED TO SEND TO US DOLLAR OUT OF TANZANIA.
TAPBTZTZ 36144524 CITY BANK N.A
111 WALL STREET 99, FLOW 19
New York /10043
Swift code: CITIVS 33

Friday, March 15, 2013

Mabadiliko ya tabia ya nchi, chanzo cha njaa Somalia

Eneo lililokumbwa na janga la njaa Somalia
Utafiti unaonyesha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotokana na shughuli za kibinaadamu ni kati ya sabau za kutonyesha mvua za kutosha Afrika Mashariki mwaka 2011 na hivyo ongezeko la joto duniani limetajwa kuwa chanzo cha njaa nchini Somalia.
Hii ni mara ya kwanza kwa mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change) kutajwa kuwa moja ya sababu za kuwepo janga la njaa. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Idara ya Hali ya Hewa Uingereza kuhusu mwenendo wa hali ya hewa Somalia mwaka 2010 na 2011, msimu wa mvua fupi ulifeli mwishoni mwa mwaka 2010 kutokana na sababu za kimaumbile za tukio la La Nina. Lakini sababu ya ukosefu wa mvua za masika mapema mwaka 2011 ilikuwa ni ongezeko la joto duniani,

Nyama ya ng'ombe yachanganywa na ya nguruwe Norway


Nyama katika supermarket barani Ulaya
Maafisa wa kitengo cha kusimamia na kukagua bidhaa nchini Norway wamegundua kuwepo kwa nyama ya nguruwe iliyochanganywa na nyama halali nchini humo. Catherine Signe Svinland Mshauri wa Kitengo cha kusimamia na kukagua bidhaa nchini Norway amesema kuwa, kimegunduliwa kiasi cha asilimia 5 hadi 30 ya nyama ya ngurume kwenye nyama ya ng'ombe ambayo imeandikwa kuwa halali kwenye maduka kadhaa nchini humo. Amesisitiza kuwa kiwango hicho cha nyama ya nguruwe hakikuwekwa kwa bahati mbaya kwenye nyama halali. Amesema kuwa, wakaguzi hao pia wamegundua kwenye sehemu inayouzwa Pizza kukiwa na nyama ya ng'ombe lakini imechanganywa kwa asilimia 60 na nyama ya nguruwe.

Sunday, March 10, 2013

Wanamisri watakiwa kuheshimu katiba ya nchi


Wanamisri watakiwa kuheshimu katiba ya nchi
Msemaji wa serikali ya Misri amesisitiza udharura wa kuheshimiwa katiba ya nchi hiyo. Alaa al Hadidi msemaji wa Waziri Mkuu wa Misri sambamba na kusisitiza udharura wa watu wote kuheshimu sheria na katiba ya nchi hiyo amewataka Wamisri, kutanguliza mbele maslahi ya kitaifa kuliko ya makundi yao binafsi na kujiepusha kuharibu miundombinu na majengo nchini humo. Al Hadidi amesema, haki ya kujieleza na kuandamana kwa amani nchini Misri inapaswa kuheshimiwa lakini wakati huo huo ameyataka makundi yote ya nchi hiyo kuacha kuharibu miundombinu na kuchoma moto majengo ya serikali na yasiyokuwa ya serikali.
Kwa siku kadhaa miji tofauti ya Misri imeshuhudia vurugu na makabiliano kati ya wanaounga mkono serikali na wanaoipinga, huku baadhi ya vikundi vikichoma moto maeneo ya umma na majengo ya serikali.

Wanajeshi wa DRC walionajisi wanawake kukamatwa


Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoWaziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Alexandre Luba Ntambo amesema atachunguza taarifa kuwa wanajeshi wa serikali walihusika na uhalifu wa kuwanajisi wanawake mwezi Novemba mwaka jana mashariki mwa nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi habari mjini Kinshasa siku ya Jumamosi, Ntambo amesema wizara yake haitavumilia utovu wa nidhamu jeshini na kwamba wanajeshi wanaohusika na vitendo vya uhalifu watachukuliwa hatua kali.
Alkhamisi iliyopita kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kilitishia kutoshirikiana na batalioni mbili za jeshi la nchi hiyo hadi pale watakapofikishwa mahakamani wanajeshi wanaotuhumiwa kuhusika na kunajisi wanawake mashariki mwa nchi hiyo.
Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema batalioni hizo mbili zimetakiwa kuwafungulia mashtaka askari waliowanajisi wanawake katika mji wa Minova.

Uhuru Kenyatta achaguliwa kuwa rais wa Kenya


Uhuru Kenyatta achaguliwa kuwa rais wa Kenya  Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kiti cha rais katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya Muungano Jubilee ameshinda uchaguzi huo katika mchuano mkali na mpinzani wake Raila Odinga wa mrengo wa Cord. Uhuru Kenyatta amepata asilimia 50.07 na mpinzani wake wa karibu yaani Waziri Mkuu Raila Odinga amepata asilimia 43.28 ya kura zote.
Uhuru ni mwana wa Jomo Kenyatta shujaa wa ukombozi wa Kenya, na sasa anashika hatamu za kuongoza Kenya baada miaka 50 tangu nchi hiyo ipate uhuru.  Uhuru Kenyatta ameweza kumshinda mpinzani wake mkuu Raila Odinga kwa kumpita kwa kura laki nane katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 4 mwezi huu. Mchuano mkali uliokuwepo kati ya wagombea hao wawili uliwafanya weledi wa mambo watabiri uwezekano wa uchaguzi huo kuingia katika duru ya pili hapo tarehe 11 mwezi Aprili. 

Saturday, March 9, 2013

Kamanda wa Kutuliza Ghasia Misri atimuliwa kazi

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri Meja Jenerali Muhammad Ibrahim al Juma'a
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri amemtimua kazi Meja Jenerali Majid Nouh Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini humo. Meja Jenerali Muhammad Ibrahim al Juma'a amemtimua kazi Meja Jenerali Majid Nouh na badala yake amemteua Meja Jenerali Ashraf Abdullah kuziba nafasi hiyo. Siku ya Alhamisi iliyopita, mamia ya polisi wa Misri walifanya mgomo na kutaka  aondolewe Waziri wa Mambo ya Ndani  wa nchi hiyo. Polisi wa Misri wanamtuhumu waziri  huyo kuwa alitumia kikosi cha usalama kwa shabaha ya kufikia  malengo yake ya kisiasa. Kwa upande mwengine, jeshi la polisi katika mji wa Port Said nchini Misri limekabidhi ulinzi wa usalama wa mji huo kwa jeshi la nchi hiyo ili kukabiliana na ghasia na machafuko ya barabarani yanayoendelea mjini humo kwa siku kadhaa sasa.

Mamilioni walalamikia marufuku ya hijabu Uturuki


Mamilioni walalamikia marufuku ya hijabu Uturuki
Zaidi ya watu milioni 12 wametaka iondoshwe marufuku ya hijabu nchini Uturuki. Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi  Serikalini  nchini Uturuki amesema kuwa, jumla ya watu milioni 12 wanapinga kuendelezwa marufuku ya hijabu  mashuleni  na hata kunyimwa  ajira wanawake wanaovaa hijabu kwenye sekta za serikali nchini humo. Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi Serikalini nchini Uturuki  amewasilisha ombi hilo kwa Waziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii wa Uturuki jumla ya saini za watu milioni 12 wanaotaka kuondoshwa marufuku ya hijabu nchini humo. Waziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii wa Uturuki ameahidi kulipeleka ombi hilo mbele ya kikao cha baraza la mawaziri nchini humo ili lijadiliwe upya.

Yemen yaiomba radhi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Yemen yaiomba radhi Jamhuri ya Kiislamu ya IranWizara ya Mambo ya Ndani ya Yemn imeiomba radhi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutoa taarifa za uwongo kwamba, Yemen imekamata meli ya Kiirani iliyokuwa imebeba shehena kubwa ya silaha. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemen imesema kuwa, inasikitishwa  na inakadhibisha taarifa zilizotangazwa nchini humo  juu ya kukamatwa  meli ya Kiirani iliyokuwa imesheheni silaha. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 2 Februari mwaka 2013, serikali ya Yemen ilidai kwamba meli moja ya Kiirani imekamatwa kwenye bandari ya Mukala nchini humo ikiwa imebeba shehena kubwa ya silaha.

Vikosi vya usalama Bahrain vyawatesa wanawake

Vikosi vya usalama Bahrain vyawatesa wanawake
Kanali ya Televisheni ya al Manar ya nchini Lebanon imeripoti kuwa,  wanawake 11 wameuawa shahidi  katika  harakati za mapinduzi ya wananchi wa Bahrain, na wengine 230 wanakabiliwa na mateso na ukandamizaji mkubwa  kwenye jela za kuogofya za utawala wa Aal Khalifa nchini humo. Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya tarehe 8 Machi ya kila mwaka kuwa ni siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa Bahrain wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha na kukiukwa  haki zao nchini humo. Taasisi ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Bahrain imeeleza kuwa, mara baada ya kuanza harakati za kimapinduzi nchini humo mwezi Februari mwaka 2011,

Thursday, March 7, 2013

Berlusconi asukumwa jela mwaka 1 nchini Italia


Berlusconi asukumwa jela mwaka 1 nchini ItaliaMahakama moja nchini Italia imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya gazeti lake kupatikana na hatia ya kuchapisha habari ya siri kuhusu shughuli za benki. Hata hivyo, mawakili wa Berlusconi wamesema kiongozi huyo wa zamani hatosukumwa jela hadi rufaa aliyokata itakaposikizwa na kuamuliwa. Iwapo atashindwa kujinasua kutoka kwenye mtego huo, hali ya kisiasa nchini Italia itakuwa chachu kutokana na ukweli kwamba, chama cha Berlusconi ni miongoni mwa vyama vinavyotarajiwa kushirikishwa kwenye serikali ya muungano baada ya wagombea wa wadhifa wa Waziri Mkuu kushindwa kupata ushindi mutlaki kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Macky Sall ataka Madrasa za Kiislamu kuboreshwa


Macky Sall ataka Madrasa za Kiislamu kuboreshwaRais wa Senegal Macky Sall, ametoa wito wa kuimarishwa Madrasa za Kiislamu nchini humo. Sall anasema kuwa serikali itafunga Madrasa zote ambazo zitakosa kutimiza mahitaji ya usalama kwa watoto. Matamshi yake Rais Macky Sall, yanajiri baada ya watoto tisa kufariki kwenye ajali ya moto katika Madrasa moja iliyoko karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Dakar. Moto huo, ulizuka wakati watoto 45 wa kati ya umri wa miaka 6 na 12, wakiwa ndani ya chumba kimoja katika eneo la Medina. Inaarifiwa kuwa huenda mshumaa ndio uliosababisha ajali hiyo ya moto uliozuka mwanzoni mwa wiki hii. Baada ya kutembele eneo kulikotokea mkasa huo hapo jana, bwana Sall, amesema kuwa shule za mafunzo ya kidini ambazo zinawadhulumu watoto na kukosa kuhakikisha usalama wao, lazima zifungwe. Kumekuwa na tuhuma kwamba baadhi ya waalimu wa Madrasa hutumia shule hizo za kidini kujitajirisha.

CORD yataka zoezi la kuhesabu kura lisimamishwe


CORD yataka zoezi la kuhesabu kura lisimamishweNchini Kenya, muungano wa CORD unaoongozwa na Waziri Mkuu Raila Odinga umetaka zoezi la kuhesabu kura za urais lisimamishwe kwa madai kwamba Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imepoteza dira katika zoezi hilo. Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Bw. Odinga amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kwamba, IEBC inafaa kuwajibikia kazi mbovu katika zoezi la kuhesabu kura. Musyoka amesema CORD haina imani na zoezi hilo na hivyo linapaswa kusimamishwa mara moja. Hata hivyo,

Somalia: Waasi watakaojisalimisha wataingia jeshini


Somalia: Waasi watakaojisalimisha wataingia jeshini
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema yuko tayari kuwajumuisha wanachama wa kundi la Al-shabab katika jeshi la taifa iwapo wataamua kuweka silaha chini na kujisalimisha kwa serikali. Rais Hassan amesema nchi inamhitaji kila Msomali ili iweze kusimama wima na kujiunga tena na nchi zingine za dunia. Kiongozi huyo pia amelishukuru Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuiondolea nchi yake vikwazo vya silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesema fursa hiyo itaiwezesha Mogadishu kujiimarisha zaidi kiusalama. Rais Hassan pia amezungumzia hali ya taasisi muhimu nchini Somalia na kusema kuwa baadhi ya taasisi kama vile idara ya mahakama ni dhaifu na ameitaka jamii ya kimataifa kusaidia kuinua hadhi ya taasisi hizo.

'US, Israel zapanga kuteka maeneo ya mafuta Sudan'


'US, Israel zapanga kuteka maeneo ya mafuta Sudan'Chama tawala cha Kongresi ya Taifa Sudan kimefichua kuwepo njama za mashirika ya kijasusi ya Marekani na Utawala wa Kizayuni ya Israel za kuwaunga mkono waasi nchini Sudan lengo likiwa ni kuyakalia kwa mabavu maeneo yenye utajiri wa mafuta nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, chama hicho tawala nchini Sudan kimesema majasusi wa Israel na Marekani wanaunga mkono makundi ya waasi hasa kundi la JEM la Darfur. Chama cha Kongresi ya Taifa kimesema pamoja na kuwepo oparesheni hizo za majasusi wa Kizayuni na Marekani,

Tuesday, March 5, 2013

Kiongozi Muadhamu: Uislamu unahimiza kupanda miti


Kiongozi Muadhamu akipanda mche mjini Tehran kwa mnasaba wa ‘Wiki ya Mazingira na Kupanda Miti’ Machi 05 2013Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja mimea na miti kuwa chimbuko la ustawi na Baraka kwa nchi zote na jamii ya mwanaadamu.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo Jumanne mjini Tehran kwa mnasaba wa ‘Wiki ya Mazingira na Kupanda Miti’. Baada ya kupanda miche miwili, Kiongozi Muadhamu amesema kuwa kulinda miti na kuzuia uharibifu wa miti ni kati ya mambo yaliyosisitizwa katika dini tukufu ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuhusu udharura wa kuwepo azma na irada imara ya kuzuia unyakuzi wa maeneo yenye misitu kando ya miji mikubwa. Amesema,

Vurugu za kidini zaikumba shule Iringa, Tanzania


Vurugu za kidini zaikumba shule Iringa, Tanzania
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bwana Shaaban Nsute. Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni na kuendelea hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo. Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata mkuu wa shule hiyo Bwana Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bwana Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake. Nsute alisema vurugu hizo ambazo zimedhibitiwa pia na Jeshi la Polisi zilizuka wakati mwanafunzi mmoja wa Kiislamu aliyevaa kofia ya kidini kudhalilishwa na mlinzi wa shuleni hiyo.