Maafisa wa kitengo cha kusimamia na kukagua bidhaa nchini Norway
wamegundua kuwepo kwa nyama ya nguruwe iliyochanganywa na nyama halali
nchini humo. Catherine Signe Svinland Mshauri wa Kitengo cha kusimamia
na kukagua bidhaa nchini Norway amesema kuwa, kimegunduliwa kiasi cha
asilimia 5 hadi 30 ya nyama ya ngurume kwenye nyama ya ng'ombe ambayo
imeandikwa kuwa halali kwenye maduka kadhaa nchini humo. Amesisitiza
kuwa kiwango hicho cha nyama ya nguruwe hakikuwekwa kwa bahati mbaya
kwenye nyama halali. Amesema kuwa, wakaguzi hao pia wamegundua kwenye
sehemu inayouzwa Pizza kukiwa na nyama ya ng'ombe lakini imechanganywa
kwa asilimia 60 na nyama ya nguruwe.
Kwa upande mwengine, siku ya Alhamisi, maafisa wa ukaguzi nchini Uingereza waligundua masalio ya nyama ya nguruwe kwenye soseji ya kuku kwenye mkahawa ulioko kwenye shule moja mjini London. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wiki chache zilizopita, kuliibuka kashfa kubwa ya uuzwaji na usambazwaji wa nyama ya farasi katika nchi mbalimbali za Ulaya. Imeelezwa kuwa, sababu ya kuuzwa nyama ya farasi badala ya ng'ombe katika nchi kadhaa za Ulaya, inatokana na urahisi wa bei ya nyama ya farasi. Amma kashfa hiyo imezusha mgogoro mkubwa wa kiafya, kwani duru za kitiba zinaeleza kwamba nyama ya farasi ina mada za sumu.

No comments:
Post a Comment