Polisi ya Misri imesema kuwa imemtia
mbaroni binamu na aliyekuwa mpambe wa karibu wa Muammar Gaddafi
kiongozi wa zamani wa Libya. Hapo jana maafisa wa Misri walisema kuwa
Ahmed Gaddaf al Dam alitiwa nguvuni baada ya vikosi vya usalama
kuizingira nyumba yake katika kitongoji cha Zamalek huko Cairo. Afisa
mmoja wa Misri amesema kuwa afisa huyo wa zamani wa intelijinsia wa
utawala wa Gaddafi atakabidhiwa kwa maafisa wa Libya hivi karibuni.
Baada ya kuzingirwa nyumba yake kwa masaa kadhaa huko katikati mwa
Cairo, binamu huyo wa Muammar Gaddafi alisikika akizungumza na kanali
moja ya televisheni kwa njia ya simu na hapa ninamnukuu" tulifika hapa
kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na baraza la kijeshi,
sisi si magaidi wa kuweza kushambuliwa namna hii," mwisho wa kumnukuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment