Mahakama moja nchini Italia imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani wa
Italia, Silvio Berlusconi kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya gazeti
lake kupatikana na hatia ya kuchapisha habari ya siri kuhusu shughuli za
benki. Hata hivyo, mawakili wa Berlusconi wamesema kiongozi huyo wa
zamani hatosukumwa jela hadi rufaa aliyokata itakaposikizwa na
kuamuliwa. Iwapo atashindwa kujinasua kutoka kwenye mtego huo, hali ya
kisiasa nchini Italia itakuwa chachu kutokana na ukweli kwamba, chama
cha Berlusconi ni miongoni mwa vyama vinavyotarajiwa kushirikishwa
kwenye serikali ya muungano baada ya wagombea wa wadhifa wa Waziri Mkuu
kushindwa kupata ushindi mutlaki kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment