Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, March 15, 2013

Mabadiliko ya tabia ya nchi, chanzo cha njaa Somalia

Eneo lililokumbwa na janga la njaa Somalia
Utafiti unaonyesha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotokana na shughuli za kibinaadamu ni kati ya sabau za kutonyesha mvua za kutosha Afrika Mashariki mwaka 2011 na hivyo ongezeko la joto duniani limetajwa kuwa chanzo cha njaa nchini Somalia.
Hii ni mara ya kwanza kwa mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change) kutajwa kuwa moja ya sababu za kuwepo janga la njaa. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Idara ya Hali ya Hewa Uingereza kuhusu mwenendo wa hali ya hewa Somalia mwaka 2010 na 2011, msimu wa mvua fupi ulifeli mwishoni mwa mwaka 2010 kutokana na sababu za kimaumbile za tukio la La Nina. Lakini sababu ya ukosefu wa mvua za masika mapema mwaka 2011 ilikuwa ni ongezeko la joto duniani,
amesema Peter Scott wa Idara ya Hali ya Hewa Uingereza (Met Office). Mashirika ya kutoa misaada yanakadiria kuwa kati ya watu 50 elfu hadi laki moja walipoteza maisha kutokana na njaa baada ya kufeli mvua. Ethiopia na Kenya pia ziliathiriwa vibaya na ukosefu wa mvua mwaka 2011. Utafiti huo haukuweza kubaini ni vipi mabadiliko ya tabia ya nchi yataathiri mvua nchini Somalia katika siku za usoni lakini suala hilo tayari limewatia wasi wasi watu wa Somalia na Afrika Mashariki kwa jumla ambao wanasema mvua hazitabiriki tena.

No comments:

Post a Comment