Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, March 5, 2013

Kiongozi Muadhamu: Uislamu unahimiza kupanda miti


Kiongozi Muadhamu akipanda mche mjini Tehran kwa mnasaba wa ‘Wiki ya Mazingira na Kupanda Miti’ Machi 05 2013Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja mimea na miti kuwa chimbuko la ustawi na Baraka kwa nchi zote na jamii ya mwanaadamu.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo Jumanne mjini Tehran kwa mnasaba wa ‘Wiki ya Mazingira na Kupanda Miti’. Baada ya kupanda miche miwili, Kiongozi Muadhamu amesema kuwa kulinda miti na kuzuia uharibifu wa miti ni kati ya mambo yaliyosisitizwa katika dini tukufu ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuhusu udharura wa kuwepo azma na irada imara ya kuzuia unyakuzi wa maeneo yenye misitu kando ya miji mikubwa. Amesema,
malalamiko yake kwa wanaoshusika na masuala ya miti na upandaji miti ni kuwa mamia ya miti inakatwa katika maeneo ambayo haipaswi kukatwa. Kiongozi Muadhamu amesema kuharibiwa maeneo ya kijani katika vitongoji vya miji hasa misitu ni mambo ambayo yanamsababishia mwanaadamu matatizo mengi na hivyo wahusika wote nchini Iran wanapaswa kuchukua hatua za kuzuia uharibifu wa misitu. Wakati huo huo Rais Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran naye pia ameongeza shughuli ya kupanda miti katika Ikulu ya Rais mjini Tehran. Katika shughuli hiyo mabalozi na wawakilishi wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM wamepanda miti katika ‘Bustani ya NAM’ iliyoko kwenye viwanja vya Ikulu hapa mjini Tehran.

No comments:

Post a Comment