Kanali ya Televisheni ya al Manar ya nchini Lebanon imeripoti
kuwa, wanawake 11 wameuawa shahidi katika harakati za mapinduzi ya
wananchi wa Bahrain, na wengine 230 wanakabiliwa na mateso na
ukandamizaji mkubwa kwenye jela za kuogofya za utawala wa Aal Khalifa
nchini humo. Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya tarehe 8 Machi ya
kila mwaka kuwa ni siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa Bahrain
wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha na kukiukwa haki zao nchini
humo. Taasisi ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Bahrain imeeleza kuwa,
mara baada ya kuanza harakati za kimapinduzi nchini humo mwezi Februari
mwaka 2011,
mashinikizo makubwa yaliwekwa dhidi ya wanawake na haki zao zimekuwa zikikanyagwa siku hadi siku. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, jumla ya wanawake 230 hivi sasa wanashikiliwa ndani ya jela za Bahrain wakikabiliwa na mateso makubwa ya kupigwa na hata kuchomwa vitu vyenye ncha kali. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanawake na watoto wadogo walipoteza maisha kwenye maandamano baada ya kurushiwa mabomu yenye gesi ya sumu na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment