Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, March 5, 2013

Vurugu za kidini zaikumba shule Iringa, Tanzania


Vurugu za kidini zaikumba shule Iringa, Tanzania
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bwana Shaaban Nsute. Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni na kuendelea hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo. Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata mkuu wa shule hiyo Bwana Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bwana Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake. Nsute alisema vurugu hizo ambazo zimedhibitiwa pia na Jeshi la Polisi zilizuka wakati mwanafunzi mmoja wa Kiislamu aliyevaa kofia ya kidini kudhalilishwa na mlinzi wa shuleni hiyo.
Alisema mlinzi wa shule hiyo, Bwana Luhala alimnyang'anya kofia hiyo ili asiingie nayo darasani kwa madai kwamba si sare ya shule. Aliongeza kuwa, kutokana na vurugu hizo zaidi ya wanafunzi 30 wamefukuzwa shuleni hapo wakiwamo wa kidato cha nne na tano hapo. Mwanafunzi aliyenyang'anywa kofia alidai kuwa, Waislamu katika shule hii wanatengwa, kunyanyaswa na kuzuiwa wasifanye mambo yanayoendana na dini yao. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Letisia Warioba, ametangaza kusikitishwa kwake na tukio hilo na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kufika mapema katika eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment