Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Alexandre
Luba Ntambo amesema atachunguza taarifa kuwa wanajeshi wa serikali
walihusika na uhalifu wa kuwanajisi wanawake mwezi Novemba mwaka jana
mashariki mwa nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi habari mjini Kinshasa siku ya Jumamosi, Ntambo amesema wizara yake haitavumilia utovu wa nidhamu jeshini na kwamba wanajeshi wanaohusika na vitendo vya uhalifu watachukuliwa hatua kali.
Alkhamisi iliyopita kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kilitishia kutoshirikiana na batalioni mbili za jeshi la nchi hiyo hadi pale watakapofikishwa mahakamani wanajeshi wanaotuhumiwa kuhusika na kunajisi wanawake mashariki mwa nchi hiyo.
Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema batalioni hizo mbili zimetakiwa kuwafungulia mashtaka askari waliowanajisi wanawake katika mji wa Minova.

No comments:
Post a Comment