Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, March 18, 2013

Wayemen waanza mazungumzo ya kitaifa

Wayemen waanza mazungumzo ya kitaifaYemen imefungua mazugumzo ya maridhiano ya kitaifa yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa ili kuandaa uwanja wa kufanyika uchaguzi na kutungwa katiba mpya kwa shabaha ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu nchini humo.  
Mazungumzo hayo yamefunguliwa na Rais Abdrabuh Mansur Hadi wa nchi hiyo na yanahudhuriwa na zaidi ya wawakilishi 500 kutoka vyama vya kisiasa vya Yemen. Hata hivyo mrengo wa kisiasa wa kusini umesusia mazungumzo hayo na uliitisha maandamano na mgomo katika mji wa Aden hapo jana kupinga suala hilo.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya makubaliano yaliyohitimisha utawala wa dikteta Ali Abdullah Saleh ambapo kiongozi huyo aliondoka madarakani na kukabidhi madaraka kwa Abdrabuh Mansur Hadi tarehe 27 Februari 2012.

No comments:

Post a Comment