Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, March 19, 2013

37 wafariki dunia katika ajali ya basi India


37 wafariki dunia katika ajali ya basi IndiaPolisi ya India imetangaza kuwa kwa akali watu 37 wamepoteza maisha na wengine 17  kujeruhiwa, baada ya basi la abiria walilopanda kupoteza mwelekeo na kutumbukia katika  mto wa Jagbudi magharibi mwa nchi hiyo.
Polisi ya India imeeleza kuwa, ajali hiyo mbaya imetokea mapema leo alfajiri katika wilaya ya Maharashtra. Polisi ya Usalama barabarani nchini India imeeleza kuwa, basi hilo lilikuwa likitokea katika mji wa Goa na kuelekea Mumbai; na kwamba  dereva wa basi hilo alishindwa kulidhibiti na kutumbukia mtoni. Polisi imeeleza kuwa, ajali hiyo imetokea umbali wa kilomita 350 kusini mwa Mumbai.
Polisi imeeleza kuwa, watu wasiopungua 17 wamejeruhiwa akiwemo dereva wa basi hilo, ambaye hali yake imeelezwa kuwa ni mahututi. Taarifa za awali zinasema kuwa, ndani ya basi hilo kulikuwa na idadi kadhaa ya watalii kutoka nje ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment