Msemaji wa serikali ya Misri amesisitiza udharura wa kuheshimiwa
katiba ya nchi hiyo. Alaa al Hadidi msemaji wa Waziri Mkuu wa Misri
sambamba na kusisitiza udharura wa watu wote kuheshimu sheria na katiba
ya nchi hiyo amewataka Wamisri, kutanguliza mbele maslahi ya kitaifa
kuliko ya makundi yao binafsi na kujiepusha kuharibu miundombinu na
majengo nchini humo. Al Hadidi amesema, haki ya kujieleza na kuandamana
kwa amani nchini Misri inapaswa kuheshimiwa lakini wakati huo huo
ameyataka makundi yote ya nchi hiyo kuacha kuharibu miundombinu na
kuchoma moto majengo ya serikali na yasiyokuwa ya serikali.
Kwa siku kadhaa miji tofauti ya Misri imeshuhudia vurugu na makabiliano kati ya wanaounga mkono serikali na wanaoipinga, huku baadhi ya vikundi vikichoma moto maeneo ya umma na majengo ya serikali.
Kwa siku kadhaa miji tofauti ya Misri imeshuhudia vurugu na makabiliano kati ya wanaounga mkono serikali na wanaoipinga, huku baadhi ya vikundi vikichoma moto maeneo ya umma na majengo ya serikali.
No comments:
Post a Comment