Rwanda imekataa kutoa viza kwa
maafisa wawili wa timu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliyoituhumu
Kigali mwaka jana kuwa inawapa silaha waasi wa mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na kuwataja kuwa watu wenye upendeleo.
Mwanadiplomasia wa Rwanda amethibitisha hatua ya nchi hiyo ya kukataa
kuwapa viza wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa kwa jina la Bernad Leloup
wa Ubelgiji na Marie Plamadiala wa Moldova. Kundi la wataalamu wa
uchunguzi kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalosimamia
utekelezaji wa vikwazo vya silaha na vingine dhidi ya Kongo lilisema
katika ripoti yake ya mwaka jana kuwa Waziri wa Ulinzi wa Rwanda alikuwa
akiamuru uasi wa kundi la M23 huko Congo na kwamba Rwanda pia ilikuwa
ikiwapa silaha waasi wa kundi hilo sambamba na kuwasaidia wanajeshi wa
kushirikiana nao katika mapigano. Kundi la wataalamu la uchunguzi kutoka
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliituhumu pia Uganda kuwa
inawaunga mkono waasi wa Machi 23. Rwanda na Uganda zote zimekanusha
tuhuma hizo dhidi yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment