Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, March 19, 2013

Siasa za Wamagharibi ni za kindumakuwili


Siasa za  Wamagharibi ni za kindumakuwili
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi ya Bahrain amezikosoa vikali siasa za kindumakuwili za Magharibi kuhusiana na matukio ya kieneo na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Bahrain unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa wa nchi hiyo.
Saeed al Shahabi ameongozana na maelfu ya wapinzani wa Bahrain na kukusanyika mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza mjini London na kusema kuwa, uungaji mkono wa kibubusa wa Marekani na Uingereza kwa utawala wa Aal Khalifa umesababisha utawala huo kuvimba kichwa na kupuuza misingi ya haki za binadamu.
Ameongeza kuwa, siasa za kindumakuwili za nchi za Magharibi sio za kikhlaki na amebainisha kuwa, Washington na London zinapaswa kukomesha uungaji mkono wao kwa utawala wa Bahrain ambao unatenda jinai za mauaji, kuwafunga na kuwashikilia korokoroni wanaharakati na kuwatesa wananchi wa nchi hiyo wanaume na wanawake.

No comments:

Post a Comment