Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, March 18, 2013

Wafungwa wa Guantanamo waendelea kugoma kula


Wafungwa wa Guantanamo waendelea kugoma kula
Mgomo wa kula chakula unaoendelea kufanywa na wafungwa walioko katika jela ya Guantanamo umeingia katika siku ya 41 huku wataalamu wa kitiba na mawakili wanaowatetea wafungwa hao wakionya kuhusu kudhoofika kiafya kwa wafungwa zaidi ya 100 waliogoma kula chakula. Mawakili na maafisa wa tiba wameeleza kuwa wana wasiwasi na hali mbaya ya kiafya ya wafungwa hao walioanza kugoma kula chakula tangu Februari 6 mwaka huu baada ya wafanyakazi wa jela ya Guantanamo kupora vitu vya wafungwa hao zikiwemo barua, picha na nakala za kitabu kitukufu cha Qu'rani wakati walipozikagua seli zao.

Wakati huo huo msemaji wa jela ya Guantanamo Kapteni Robert Durand amesema mgomo wa kula chakula unazidi kushika kasi katika jela hiyo ambapo tarehe 15 mwezi huu alikiri kuwa idadi ya wafungwa wanaozidi kugomea chakula inaongezeka. Tarehe 14 mwezi huu mawakili 45 wanaowatetea baadhi ya wafungwa wanaoshikiliwa katika jela hiyo ya Guantanamo walimtumia barua ya wazi Chuck Hagel Waziri wa Ulinzi wa Marekani wakimtaarifu kuhusu suala hilo na kumtaka achukue hatua ili kumaliza mgomo huo.

No comments:

Post a Comment