Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri amemtimua kazi Meja Jenerali
Majid Nouh Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini humo. Meja
Jenerali Muhammad Ibrahim al Juma'a amemtimua kazi Meja Jenerali Majid
Nouh na badala yake amemteua Meja Jenerali Ashraf Abdullah kuziba nafasi
hiyo. Siku ya Alhamisi iliyopita, mamia ya polisi wa Misri walifanya
mgomo na kutaka aondolewe Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo.
Polisi wa Misri wanamtuhumu waziri huyo kuwa alitumia kikosi cha
usalama kwa shabaha ya kufikia malengo yake ya kisiasa. Kwa upande
mwengine, jeshi la polisi katika mji wa Port Said nchini Misri
limekabidhi ulinzi wa usalama wa mji huo kwa jeshi la nchi hiyo ili
kukabiliana na ghasia na machafuko ya barabarani yanayoendelea mjini
humo kwa siku kadhaa sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment