Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemn imeiomba radhi Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran kwa kutoa taarifa za uwongo kwamba, Yemen imekamata
meli ya Kiirani iliyokuwa imebeba shehena kubwa ya silaha. Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Yemen imesema kuwa, inasikitishwa na inakadhibisha
taarifa zilizotangazwa nchini humo juu ya kukamatwa meli ya Kiirani
iliyokuwa imesheheni silaha. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 2
Februari mwaka 2013, serikali ya Yemen ilidai kwamba meli moja ya
Kiirani imekamatwa kwenye bandari ya Mukala nchini humo ikiwa imebeba
shehena kubwa ya silaha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment