Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, March 7, 2013

CORD yataka zoezi la kuhesabu kura lisimamishwe


CORD yataka zoezi la kuhesabu kura lisimamishweNchini Kenya, muungano wa CORD unaoongozwa na Waziri Mkuu Raila Odinga umetaka zoezi la kuhesabu kura za urais lisimamishwe kwa madai kwamba Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imepoteza dira katika zoezi hilo. Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Bw. Odinga amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kwamba, IEBC inafaa kuwajibikia kazi mbovu katika zoezi la kuhesabu kura. Musyoka amesema CORD haina imani na zoezi hilo na hivyo linapaswa kusimamishwa mara moja. Hata hivyo,
Musyoka amewataka wafuasi wao kuwa watulivu na kusisitiza kwamba, CORD haina lengo la kuitisha maandamano ya kitaifa. Amesema viongozi wakuu wa muungano huo wanaendelea kujadiliana na huenda wakafika mahakamani kuwasilisha kilio chao. Hata hivyo mwenyekiti wa IEBC amewaambia wanahabari kwamba zoezi la kuhesabu kura litaendelea kwa kuwa hakuna sharia zilizokiukwa. Amekanusha tuhuma kwamba tume yake inashinikizwa na nchi za Magharibi kumtangaza mgombea fulani kuwa mshindi wa kiti cha urais. Hii ni katika hali ambayo, mgombea wa urais kwa tiketi ya muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta anaendelea kuongoza hadi sasa baada ya takriban asilimia 40 ya kura zote kuhesabiwa na kutangazwa.

No comments:

Post a Comment