skip to main |
skip to sidebar
Macky Sall ataka Madrasa za Kiislamu kuboreshwa
Rais wa Senegal Macky Sall, ametoa wito wa kuimarishwa
Madrasa za Kiislamu nchini humo. Sall anasema kuwa serikali itafunga
Madrasa zote ambazo zitakosa kutimiza mahitaji ya usalama kwa watoto.
Matamshi yake Rais Macky Sall, yanajiri baada ya watoto tisa kufariki
kwenye ajali ya moto katika Madrasa moja iliyoko karibu na mji mkuu wa
nchi hiyo, Dakar. Moto huo, ulizuka wakati watoto 45 wa kati ya umri wa
miaka 6 na 12, wakiwa ndani ya chumba kimoja katika eneo la Medina.
Inaarifiwa kuwa huenda mshumaa ndio uliosababisha ajali hiyo ya moto
uliozuka mwanzoni mwa wiki hii. Baada ya kutembele eneo kulikotokea
mkasa huo hapo jana, bwana Sall, amesema kuwa shule za mafunzo ya kidini
ambazo zinawadhulumu watoto na kukosa kuhakikisha usalama wao, lazima
zifungwe. Kumekuwa na tuhuma kwamba baadhi ya waalimu wa Madrasa hutumia
shule hizo za kidini kujitajirisha.
No comments:
Post a Comment