Walimu watatu wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa
na watu wenye silaha dhidi ya shule mbili huko kaskazini mashariki mwa
Nigeria. Walimu hao waliuawa jana katika mashambulio mawili
yaliyotekelezwa na watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kundi
la Boko Haram katika mji wa Maiduguri unaopatikana katika jimbo la Borno
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Aidha wanafunzi kadhaa walijeruhiwa
katika mashambulizi hayo. Kabla ya hapo pia, watu 25 waliuawa na makumi
ya wengine kujeruhiwa baada ya kutokea milipuko mitano katika mji wa
Kano kaskazini mwa Nigeria. Hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote
lililotangaza kuhusika na mashambulio hayo, lakini kundi la Boko Haram
linashukiwa kuwa ndilo lililotekeleza mashambulio hayo kwa vile limekuwa
likitekeleza mashambulio kama hayo katika maeneo tofauti ya nchi hiyo
ya Magharibi mwa Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment