Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema yuko tayari
kuwajumuisha wanachama wa kundi la Al-shabab katika jeshi la taifa iwapo
wataamua kuweka silaha chini na kujisalimisha kwa serikali. Rais Hassan
amesema nchi inamhitaji kila Msomali ili iweze kusimama wima na
kujiunga tena na nchi zingine za dunia. Kiongozi huyo pia amelishukuru
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuiondolea nchi yake vikwazo
vya silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesema fursa hiyo itaiwezesha
Mogadishu kujiimarisha zaidi kiusalama. Rais Hassan pia amezungumzia
hali ya taasisi muhimu nchini Somalia na kusema kuwa baadhi ya taasisi
kama vile idara ya mahakama ni dhaifu na ameitaka jamii ya kimataifa
kusaidia kuinua hadhi ya taasisi hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment