Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, August 30, 2013

TASWIRA ZA AJALI ILIYOUWA WATU 41 NA KUJERUHI 33 NCHINI KENYA


Pichani juu ni taswira za ajali ya basi iliyouwa watu 41 na kujeruhi 33 katika eneo la Ntulele lililo kwenye mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya. Basi hilo lilikuwa likiwasafirisha zaidi ya abiria 60 kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi kuelekea mji wa Homabay uliopo magharibi mwa Kenya lilikosa mwelekeo na kupinduka mara kadhaa usiku wa kuamkia Alhamisi. Watu 33 walifariki papo hapo huku wengine 8 wakifariki baadaye walipokuwa wakipata matibabu hospitalini. Watu wengine 33 waliopata majeraha mabaya wanaendela kupata matibabu kwenye hospitali tofauti nchini Kenya. Akituma rambirambi zake kwa familia za marehemu, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka madereva kuwa waangalifu na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kuhakikisha maisha ya Wakenya hayapotei kwa ajali za barabarani. (Picha na Nation)

Friday, August 23, 2013

Abaka, Awalawiti Watoto Akiwemo wa Kwake.


Na Joseph Ngilisho, Arusha
KATIKA hali isiyo ya kawaida baba mwenye familia, mke na watoto, David Samwel (21) mkaazi wa Moivaro, Nkwandua wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, anadaiwa kuwabaka na kuwalawiti watoto wanne wa kike wenye umri wa miaka 6 na 7, akiwemo mtoto wake wa kumzaa kwa nyakati tofauti chumbani kwake.

Mtuhumiwa alitenda unyama huo kwa kumbaka pia mtoto wa mama mwenye nyumba wakati mkewe, akiwa ameenda kwenye biashara zake za kuuza mboga na kuwaacha watoto hao wakicheza nyumbani.

Akisimulia mkasa huo, mama mwenye nyumba, (jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka 30 alisema, aligundua mwanae (jina limehifadhiwa) amebakwa wakati alipotaka kumkosha.

Alisema baada ya kumwita mtoto huyo, alikimbia na kwenda kujificha chumbani na alipomfuata aligoma kuvua nguo hali iliyomlazimu kumchapa ndipo alipomweleza alikuwa amefanyiwa mchezo mbaya na mtuhumiwa.

Baada ya kumuangalia sehemu za siri aligundua alikuwa ameharibika vibaya na sehemu zake za siri zimekuwa kama za mtu mzima, ndipo alipoamua kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika na kuanza kumhoji mtoto huyo.

Mtoto huyo alisimulia jinsi mtuhumiwa alivyokuwa akitekeleza unyama huo kwa kuwabaka pia watoto wengine wa majirani ambapo kitendo hicho amekuwa akikitekeleza baada ya kuwapaka mafuta ya alizeti sehemu zao za siri (mbele na nyuma) na kisha kuwaingilia.

Hata hivyo, mtoto wa mama huyo aliwataja wenzake wanaofanyiwa mchezo huo na walipofuatwa walikiri na baada ya kuwapeleka hospitali ya wilaya Tengeru daktari aliewapima alithitisha wameingiliwa sehemu zote ila alisema hawakuambukizwa maradhi.

Watu wenye hasira walimshambulia mtuhumiwa huyo na kisha kumfikisha kituo cha polisi Tengeru.

Akisimulia jinsi walivyokuwa wakitendwa, mmoja wa watoto hao (jina linahifadhiwa) alisema mara kwa mara mtuhumiwa alikuwa akimtuma mtoto wake wa miaka 7 awaite wenzake na wanapofika chumbani huwaamuru kuvua nguo zote na kuanza kuwaingilia mmoja baada ya mwenzake.

“Tukifika chumbani hutuambia tuvue nguo halafu anatupaka mafuta ya alizeti na kutufanya tabia mbaya, mimi na mwenzangu (akamtaja jina),tulikuwa tunasikia maumivu lakini alituambia mbona Fulani (akataja jina la mtoto wake) hasikii maumivu,”alisema.

Alisema baada ya kumaliza huwanunulia pipi na kuwapa shilingi 200 huku akiwataka wasitoe siri.

“Mara ya kwanza tulipofika chumbani kwake tuliogopa ila alimleta mtoto wake na kumfanya tabia mbaya mbele yetu huku akituambia tuangalie jinsi ambavyo mwenzao (mtoto wake) hasikii maumivu,” alisema mtoto huyo.

Naye mwenyekiti wa serikali za mitaa, Moivaro, Josephat Laizer pamoja na kukerwa na tukio hilo alisema kama watamuachia, atawahamasisha wanachukua sheria mkononi kumwadabisha mtuhumiwa.

Kwa upande wa mke wa mtuhumiwa, alisikitishwa na kitendo cha mumewe kumwingilia na kumnajisi mtoto wao wa kuzaa na kusema huenda mumewe ana pepo la ngono.

Alisema alikuwa akimpa unyumba kama kawaida tena hata mara tatu kwa usiku mmoja.

Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Askari wa UN Congo waamrishwa kulinda raia


Askari wa UN Congo waamrishwa kulinda raiaMkuu wa operesheni ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amewaamuru askari wa kulinda amani wa jeshi la umoja huo kuchukua hatua za dharura za kulinda raia katika mji wa Goma baada ya makombora kadhaa kupiga mji huo na kuua raia.
Martin Kobler amesema maeneo ya raia na vituo vya jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO vimeshambuliwa na kwamba amelitaka jeshi hilo kuchukua hatua za dharura za kuwalinda raia na kuzuia kusonga mbele wapiganaji wa kundi la M23.
Duru za habari zinasema kuwa makombora matatu yamelenga mji wa Goma na kuua watu kadhaa wakiwemo watoto wadogo mawili. Vilevile habari zinasema kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 Alkhamisi ya jana waliingia katika ukanda wa usalama unaozunguka mji wa Goma huko mashariki mwa Congo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda. Maafisa wa serikali ya Congo wanasema kundi la M23 limevurumisha makombora kadhaa katika mji wa Goma na kwamba makombora mengine yamevuka mpaka na kuingia katika ardhi ya Rwanda.
Serikali ya Kigali imelaani tukio hilo na kulilaumu jeshi la serikali ya Kinshasa kwa shambulizi hilo. Wizara ya Ulinzi ya Rwanda imesema shambulizi hilo haliwezi kuhalalishwa kwa njia yoyote ile.

Keita: Uislamu utumike kuleta maelewano Mali


Keita: Uislamu utumike kuleta maelewano MaliRais mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametoa wito kwa watu wote nchini humo kushikamana na misingi na thamani za Kiislamu ili kuleta umoja na maelewano ya kitaifa.
Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako kwa mara ya kwanza baada ya ushindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni, Keita alisema mambo atakayoyapa umuhimu ni utawala wa kisheria, kuliimarisha jeshi  na kupambana na ufisadi.
Keita amesisitiza kuwa yeye atakuwa rais wa watu wote wa Mali na kwamba sasa hakuna haja tena ya uhasama baina ya makundi mbali mbali nchini humo. Ibrahim Boubacar Keita ambaye ataapishwa mwezi ujao wa Septemba amesema hivi sasa Mali inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinaweza kutatuliwa tu kwa kutegemea thamani za Kiislamu na kuvumiliana. Mgogoro wa Mali ulianza tarehe 22 Machi mwaka huu wakati wanajeshi waasi wakiongozwa na Amadou Sanogo walipofanya mapinduzi yaliyomng'oa madarakani Rais Amadou Toumani Toure kwa madai kuwa ameshindwa kuzima uasi kaskazini mwa nchi hiyo. Baada ya hapo waasi walichukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Hivi sasa baada ya uchaguzi utulivu umerejea nchini humo.

Kenya: Al Qaida inatayarisha shambulizi Mombasa


Kenya: Al Qaida inatayarisha shambulizi MombasaPolisi ya Kenya imetahadharisha kuwa kundi la kigaidi la al Qaida linajitayarisha kufanya mashambulizi katika mji wa pwani wa Mombasa katika kumbukumbu ya mauaji ya msomi wa Kiislamu Sheikh Aboud Rogo.
Taarifa ya polisi ya Kenya ambayo hadi sasa haijamtia nguvuni mtu aliyemuua msomi huyo wa Kiisalmu, imesema kuwa kundi la al Shabab linaloshirikiana na mtandano wa al Qaida, huenda linapanga kufanya mashambulizi ya kukumbuka kuuliwa msomi huyo.
Mkuu wa polisi ya kaunti ya Mombasa Robert Kitur amesema jeshi la polisi limepata taarifa za kipelelezi kuhusu tishio la shambulizi la kundi la al Shabab katika mji wa Mombasa katika kumbukumbu ya mauaji ya Sheikh Aboud Rogo. Kitur amesema usalama umeimarishwa zaidi katika mji wa Mombasa na kwamba polisi imezuiya maandamano ya kukumbuka tukio la kuuawa Sheikh Rogo.
Waislamu wengi wa Kenya wanaituhumi serikali ya nchi hiyo kwamba ilihusika na mauaji ya Sheikh Aboud Rogo yaliyofanyika Agousti 27 mwaka jana. Vyombo vya usalama vya Kenya hadi sasa havijamkamata mtu au watu waliofanya mauaji hayo.

Wednesday, August 21, 2013

KESI YA SHEKH PONDA YAIGHALIMU SERIKALI SHILINGI MILLIONI 1O


NewsImages/6955262.jpgUsafiri wa helikopta waitafuna dola mara 71 ya gharama ya gari
 
ULINZI wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiwa gerezani na anapopelekwa mahakamani, umeanza kuvitesa vyombo vya Dola. Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, zinaeleza kuwa serikali juzi ilitumia kiasi cha shilingi 10,682,031 kama gharama za usafiri wa helikopta za kumpeleka na kumrudisha kiongozi huyo mahakamani mkoani Morogoro.

MTANZANIA Jumatano kupitia vyanzo vyake vilivyoko ndani na nje ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 hadi saa moja ni dola za Marekani 3,000 hadi 3,300 ambazo ni sawa na shilingi 5,341,032.85 .

Hivyo gharama za kwenda na kurudi kwa saa jumla yake ni dola za Marekani 6,600 ambazo ni sawa na shilingi 10,682,031.

Akithibitisha hilo, Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, Antony Mwami alisema gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 ni dola 3,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni tano.

Katika uchunguzi wake gazeti hili limebaini kuwa gharama hizo zilizotumika kwa siku moja tu, zingetosha kumsafirisha Ponda kwenda Morogoro na kurudi mara 71, endapo ungetumika usafiri wa gari wa kawaida.

Gazeti hili limebaini kuwa kwa usafiri wa kawaida wa gari, gharama za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hazizidi shilingi 150,000.

Juzi Jeshi la Polisi kwa kutumia helikopta yake inayodaiwa kuwa na uwezo wa kubeba watu wanane, lilimsafirisha Sheikh Ponda hadi mkoani Morogoro ambako alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na kusomewa mashtaka ya uchochezi yanayomkabili.

Sheikh Ponda aliwasili kwa helikopta hiyo na kutua kwenye uwanja wa gofu, Morogoro akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na alipakiwa tena kwenye gari maalumu ambalo liliongozana na mengine matatu ya polisi kuelekea eneo la mahakamani.

Baada ya kumalizika kusomwa kwa kesi hiyo, msafara ule ule ulimrejesha uwanja wa gofu saa sita mchana na kupandishwa tena kwenye helikopta kurejea jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, gharama hizo zinazozidi shilingi milioni 10 ni zile za helikopta tu, mbali na nyingine zikiwemo posho pamoja na magari yaliyotumika kumsafirisha wakati alipotua na kurudi katika uwanja wa gofu.

MTANZANIA Jumatano limedokezwa kuwa ndani ya Jeshi la Polisi, rubani anayerusha helikopta kwa muda wa saa moja, hulipwa kuanzia shilingi 100,000.

Kwamba helikopta iliyotumika kumbeba Ponda, hubeba watu wanane kwa maana ya marubani wawili na abiria wengine sita.

Hata hivyo gazeti hili limedokezwa kuwa, kwa askari ambao wanasindikiza mahabusu kama watalala wanakokwenda, hulipwa posho na kama hawalali hawalipwi.

Katika tukio la kumsindikiza Ponda hawakulala, hivyo hawakulipwa chochote.

Wakati hayo yakijitokeza, Gazeti hili kupitia vyanzo vyake vya habari vilivyoko ndani ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa hatua ya Ponda kusafirishwa kwa helikopta ilitokana na uamuzi wa baadhi ya viongozi wa juu wa Jeshi hilo walioko Dar es Salaam na wale wa Morogoro.

Inaelezwa kuwa viongozi hao walifikia uamuzi huo, baada ya kudai kuwapo kwa taarifa za kiintelijensia za kuwapo kwa tishio la usalama wa nchi endapo Ponda angesafirishwa kwa njia ya kawaida.

Juzi Ponda alianza kwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kufutiwa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili, baada ya kusomewa mara ya kwanza Agosti 14 mwaka huu akiwa kitandani katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kumshitaki.

Alidaiwa kutenda makosa hayo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano kati ya Juni 2 na Agosti 11 mwaka huu.

Ponda alifikishwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na baadaye alipandishwa kizimbani na kufutiwa kesi hiyo baada ya Wakili Kweka kuwasilisha hati hiyo ya DPP chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Baada ya kufutiwa mashtaka hayo, alichukuliwa na kupelekwa Morogoro ambako pia alisomewa mashtaka ya uchochezi.

Huenda kiongozi wa Boko Haram 'amekufa'


Abubakar Shekau, Kiongozi wa Boko Haram
Abubakar Shekau amekua kiongozi wa Boko Haram tangu mwaka wa 2009. Kundi lake limeendesha mashambulizi ya mabomu na utekaji nyara wa raia.
Huenda kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigera, Abubakar Shekau aliuawa na maafisa wa usalama katika ufyatulianaji wa risasi. Duru za kijeshi zinasema huenda Shekau aliuawa kati ya Julai 25 na Agosti 3.
Kundi la Boko Haram ambalo limekua likiendesha maasi Kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka wa 2009 halijatoa taarifa yeyote. Marekani ilitangaza tuzo ya dola Milioni saba kwa yeyote yule angepeana taarifa za kumnasa Shekau.
Taarifa za kijasusi zinasema Shekau alipigwa risasi Juni 30 wakati jeshi la Nigeria liliposhambulia maficho ya Boko Haram katika msitu wa Sambisa Kaskazini Mashariki mwa nchi.
Shekau alipata majeraha mabaya na kuvukishwa hadi katika mji ulioko mpaka na Cameroon kwa matibabu. Inaaminika alikufa kati ya Julai 25 na Agosti tatu mwaka huu. Waandishi wa habari wamesema hakuna taarifa huru ambazo zimethibitisha kifo cha Shekau.
Maelfu ya raia wameuawa tangu Boko Haram kaunza maasi mwaka 2009. Abubakar Shekau alichukua uwongozi wa wapiganaji hao wa kiisilamu baada ya kifo cha mwanzilishi wa Boko Haram, Muhammad Yusuf aliyefariki dunia wakati akiwa kizuizini.
Kundi hilo limeendesha mashambulizi mabaya na ya kikatili wakati wa uwongozi wa Shekau. Boko Haram wamekuwa wakishinikiza kuunda taifa la Kiisilamu nchini Nigeria.
Hapo mwezi Mei mwaka huu Rais Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu Kaskaizni mwa Nigeria ambapo pia alituma jeshi kuendesha operesheni dhidi ya wapiganaji hao.
Chanzo : BBC SWAHILI 

Monday, August 19, 2013

Waziri wa serikali ya Misri ateteta mauaji ya raia


Waziri wa serikali ya Misri ateteta mauaji ya raia
Nabil Fahmy, Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya mpito ya Misri iliyowekwa madarakani na jeshi ametetea ukandamizaji na umwagaji mkubwa wa damu uliofanywa hivi karibuni na jeshi dhidi  ya wafuasi wa Muhammad Morsi, rais wa nchi hiyo aliyeng’olewa madarakani na jeshi. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Cairo Fahmy amesema serikali ya mpito imeonyesha uvumilivu katika kukabiliana na waandamanaji na itaendelea kufanya hivyo. Matamshi hayo yametolewa huku Muungano Dhidi ya Mapinduzi unaojumuisha makundi kadhaa ikiwemo harakati ya Ikhwanul Muslimin ukijipanga kufanya maandamano mapya mjini Cairo. Zaidi ya watu 800 wameuawa na maelfu kadhaa kujeruhiwa katika ukandamizaji uliofanywa na jeshi na polisi ya Misri dhidi ya maandamano yaliyofanyika siku ya Jumatano na Ijumaa katika miji kadhaa ya Misri. Wakati huohuo jumuiya kadhaa za kutetea haki za binadamu ndani na nje ya Misri zinajiandaa kuchukua hatua ya kuwasilisha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC dhidi ya Jenerali Abdulfatah al Sisi pamoja na maafisa wengine wa kijeshi na wa kiraia wa serikali ya mpito kwa kuhusika na mauaji ya hivi karibuni ya raia. Jumuiya hizo zimeeleza kuwa zinakusanya nyaraka na ushahidi ili kumfikisha katika Mahakama ya ICC Waziri wa Ulinzi al Sisi, Waziri wa Mambo ya Ndani Muhammad Ibrahim na maafisa wengine kadhaa wa jeshi…/

Wafuasi wa Sheikh Ponda wapiga kambi Segerea


Wafuasi wa Sheikh Ponda wapiga kambi Segerea
Habari zinasema kuwa wafuasi wa Sheikh Ponda Issa Ponda ambye anashikiliwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam nchini Tanzania baada ya kutoka hospitalini  wamezuiliwa kumowana kiongozi huyo wa kidini na wametishia kuinyima CCM kura katika uchaguzi wa mwaka 2015 huku Profesa Lipumba wa chama cha Cuf akitaka afutiwa mashtaka. Ofisa habari wa magereza kwa jina la Deodatus Kizinja amesema kisheria ni watu wawili tu kwa mwezi ndio wanaoruhusiwa kumwona mahabusu moja.
Wakizungumza jana nje ya gereza hilo, wafuasi hao walisema walipofika hapo saa nne asubuhi waliambiwa kuwa tayari ndugu zake wanne walikwisharuhusiwa kuingia kumwona na kwamba idadi ya watu hao waliomuona inatosha.

Mahakama ya Misri yaamuru Mubarak aachwe huru


Mahakama ya Misri yaamuru Mubarak aachwe huru
Mahakama ya Misri imeamuri dikteta Hosni Mubarak kuachiliwa huru baada ya mahakama hiyo kusema kuwa hakupatwa na hatia katika kesi iliyokuwa imebakia ya ubadhilifu. Kwa mujibu wa wakili wake na duru za mahakama za Misri, leo Jumatatu korti imeamuru Mubarak aachiliwe huru katika kesi ambayo yeye na watoto wake wawili Alaa na Gamal walikuwa wakituhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma. Taarifa hiyo inasema kwamba, Mubarak anaweza kuachiliwa huru wiki hii, lakini watoto wake wawili wataendelea kushikiliwa. Huko nyuma pia iliamriwa kwamba dikteta huyo wa Misri aachiliwe huru katika kesi nyingine mbili ambapo alishitakiwa kuhusika katika mauaji ya waandamaji wakati wa harakati za maandamano ya mwaka 2011 ambayo yalimuaondoa madarakani na pia kujilimbikizia mali kinyume cha sheria. Wamisri wengi wanaamini kuwa Mubarak aliyekuwa kibaraka mkubwa wa Marekani na Israel wakati wa utawala wake anapaswa kuhukumiwa kifo kutokana na kuwaua waandamanaji.

Wapinga mapinduzi Misri kuendelea kuandamana


Wapinga  mapinduzi Misri  kuendelea kuandamana
Muungano wa wapinga mapinduzi ya kijeshi nchini Misri umeapa kuendelea na maandamano licha ya vikosi vya usalama kuendeleza ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa Muhammad Mursi. Hii leo pia wafuasi wa Mursi wameendelea kuandamana katika mji mkuu Cairo na miji mingineyo ya nchi hiyo wakitaka kiongozi huyo aliyepinduliwa na jeshi arejeshwe madarakani. Wakati huo huo wafuasi wa Mursi wametaka kufanyike uchunguzi rasmi wa mauaji ya waandamani 36 waliokuwa wanashikiliwa na polisi yaliyotokea jana walipokuwa wakisafirishwa na gari la polisi.
 Katika upande mwingine Umoja wa Ulaya umesema kwamba, iwapo umwagaji damu haitositishwa nchini Misri , katika siku zijazo itaangalia uhusiano wake na jeshi la nchi hiyo na serikali ya mpito ya Cairo.   Hata hivyo Nabil Fahmy Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ametetea ukandamizaji mkubwa wa jeshi dhidi ya wafuasi wa Mursi huku Mkuu wa Jeshi Jenarali Abdul Fattah al Sisi akisisitiza kwamba hawatoacha kukabiliana na kile alichokitaja kuwa ni ghasia na machafuko.

Sunday, August 18, 2013

Saturday, August 17, 2013

MBIVU NA MBICHI KUHUSU HATMA YA SHEKH PONDA KUFAHAMIKA KESHO


Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetangaza mkutano wa dharura wa Waislamu jijini Dar es Salaam utakaofanyika kesho, kutafakari hatua za kuchukua kuhusu suala la Katibu wake, Sheikh Issa Ponda.
Hatua hiyo imefikia huku Jumuiya hiyo ikivilaumu vyombo vya usalama, kumuondoa Sheikh Ponda kutoka Taasisi ya Mifupa na Magonjwa ya Fahamu (Moi), akiwa hajamaliza matibabu na kumpeleka gerezani.
Aidha, jumuiya hiyo imelaumu taarifa za gazeti moja (siyo NIPASHE), kwamba Waislamu walipanga kuandamana jana, na kusema zililenga kuwachonganisha (Waislamu) na serikali.
Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajab Katimba, akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari jana kwenye msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam.
“Tunaalani kitendo cha polisi na usalama wa taifa, kutenda vitendo vinavyoashiria uonevu kwa viongozi wa dini ya kiislam, serikali itenda uadilifu kwa raia wake hata pale inapokuwa inaamini kuwa raia hao wana makosa,” alisema.
Alisema Jumuiya hiyo inashindwa kuamini kama mambo hayo yanaweza kufanywa na serikali, inayodai kutawala kwa kufuata utawala bora unaojali sheria, uadilifu, utu na uhuru wa kujieleza.
Alisema Jumuiya haikatai Sheikh Ponda kufunguliwa mashtaka lakini atendewe haki.
“Kitendo cha kumpiga risasi Sheikh Ponda na kisha kumtoa hospitalini na kumpeleka gerezani kwa kukiuka taratibu ni kinyume cha haki za binadamu, utawala bora na uhuru wa maisha ya mtu,” alisema Sheikh Katimba.
Sheikh Katimba ambaye alikuwa akisoma taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh Juma Said Ally, alisema Ponda anastahili haki ya matibabu hata kama anatuhumiwa.
Pia, alisema ufumbuzi wa suala la amani ya kweli na ya kudumu nchini ipo katika kushughulikia madai ya msingi ya Waislamu dhidi ya serikali, akisema ndiyo chanzo cha Sheikh Ponda, kupigwa risasi.
Sheikh Katimba, mkutano wa kesho utafanyika katika viwanja vya Nurul Yakin saa 9:00 alasiri, ambapo watatafakari na hatimaye kuchukua hatua za msingi zitakazoleta tija ya kweli ili viongozi wa kiislamu wasiendelee kudhalilishwa.
Naye Amiri Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha, alisema Waislamu hawana mpango wa kufanya maandamano kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Juzi, Sheikh Ponda, aliondolewa MOI alikokuwa akipata matibabu kufuatia kujeruhiwa mkoani Morogoro, ikiwa ni siku moja baada ya kusomewa mashtaka ya uchochezi akiwa kitandani.
Akizungumza na NIPASHE juzi muda mfupi baada ya tukio hilo, mke wa Sheikh Ponda, Khadija Ahmad, alisema saa 4:00 asubuhi, aliingia daktari ambaye hajawahi kumuona kwa kuwa siye aliyekuwa akimtibu mumewe.
Alisema daktari huyo alimwangalia mumewe kwa muda mfupi kisha akawaeleza kuwa mgonjwa anaendelea vizuri, hivyo ameamua kumruhusu.
Kwa mujibu wa Khadija, walipinga jambo hilo kwa kuwa hali ya mumewe waliona kuwa ilikuwa bado haijatengamaa.
Hata hivyo, alisema daktari huyo alishikilia msimamo wake na kutoka nje ya chumba alicholazwa Sheikh Ponda.
Alisema baada ya muda mfupi, waliingia askari kanzu wengi na kumchukua Sheikh Ponda bila kusema wanakompeleka. 
 
SOURCE::: NIPASHE

MAAJABU MAAJABU:MWANAMKE AJIFUNGUA CHURA WILAYANI CHUNYA


Mtoto aliyezaliwa pamoja na kiumbe cha ajabu kinachofanana na chura
Hiki ndicho kiumbe kilchotoka tumboni pamoja na mtoto mchanga kwa mama Matrida picha hii mara baada ya kutenganishwa na mtoto huyo
Kushoto ni Matrida Erick (20) aliyejifungua mtoto pamoja na kiumbe hicho cha ajabu akiwa na mkunga Agripina Sikanyika aliyembeba mtoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kujifungua kwa mkunga huyo.
Hapa ndipo  kwa mkunga Agripina Sikanyika Matrida alipojifungulia watoto hao
Mkunga huyo akionyesha mkeka unaotumika kuwatandikia wajawazito wanaokuja kujifungulia katika  kliniki yake
MKUNGA akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la MATRIDA ERICK  mwenye umri wa miaka ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya chunya ,amejifungua mtoto jinsi ya kiume na wakati huohuo na chura.
Mkunga aliyemzalisha bi AGGRIPINA SIKANYIKA mkazi wa MBUYUNI wilaya ya chunya amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alasiri agosti 13 mwaka huu,mara  mwanamke huyo kufikishwa kwa mkunga huyo na mumewe aitwaye BUNDALA JOSEPHAT ISANDU mwenye umri wa miaka thelathini na tano
MATRIDA amesema huo ni uzao wake wanne  na kwamba alishangazwa na kiumbe hicho ingawa wakati anajifungua hakupata tatizo  lolote na pia alifurahia kupata mtoto wa kiume mwenye afya na alisikitishwa kupata hicho kiumbe ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye vidole vinne na miguu ya nyuma vidole vitano vya binadamu.
Kwa upande wake AGGRIPINA amesema mtoto alikuwa katika kondo lake na chura alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa mwanamke huyo na pia ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la kwanza  mwanamke alijifungua kichwa cha ng’ombe mwaka jana na la pili mwaka huu mwezi wa tano ambapo mwanamke alijifungua chura badala ya binadamu kwa hiyo hili ni tukio la tatu hivyo hakushangazwa na tukio hilo.
Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia yao hilo ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa kijiji cha MBUYUNI bwana CONRAD WAMBOKA ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji MICHAEL SANZIMWA ambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo kuondoa kiumbe hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.
Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae ambapo ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani za kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya.
Na Ezekiel Kamanga  Mbeya yetu

Friday, August 16, 2013

MWAKYEMBE: NITAANIKA VIGOGO WA ‘UNGA’ LEO



Siku moja baada ya kufanya ziara ya ghafla Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema leo ataweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini.

Dk Mwakyembe juzi alifanya ziara hiyo JNIA kukagua utendaji kazi kwenye uwanja huo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kashfa ya kupitishwa kwa dawa za kulevya na baadhi ya Watanzania wakiwamo wasanii kukamatwa sehemu mbalimbali duniani.

Aidha, hatua ya waziri huyo imekuja siku tatu baada ya ahadi aliyotoa akiwa Mwanza kwamba katika kipindi cha wiki mbili kuanzia juzi, atahakikisha anawakamata vigogo wote walio katika mtandao wa usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vyote vya ndege nchini.

Akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya Jitambue Foundation, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana, Dk Mwakyembe alisema yuko tayari kufa katika vita hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana, Dk Mwakyembe alisema: “Kesho (leo) nitawataja wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kwa sasa nakamilisha ushahidi wa kutosha ikiwa ni pamoja na picha za wahusika.”

Aliwaonyesha waandishi wa habari picha ya mtuhumiwa mmoja ambaye alisema alikamatwa saa nane baada ya waziri huyo kufanya ziara uwanjani hapo. “Ninataka watu wafahamu wanaoliingiza taifa hili katika aibu hii, ambayo inasababisha Watanzania wasiaminike katika viwanja vya ndege vya mataifa mengine.”

“Hatuwezi kuwa taifa la kuogopaogopa, hii ni vita ya kusafisha nchi yetu, kwani ni nani mwenye mkataba na Mungu kuwa ataishi milele?” alihoji Waziri huyo alipokuwa akijibu swali kuwa suala la kuwataja watu wanaowafichua wasafirisha unga linaweza likaweka rehani maisha yake.

“Kama hupendi joto usiingie jikoni”, alisema.

Akizungumzia watendaji wa JNIA kuhusiana na dawa za kulevya, alisema: “Mfanyakazi yeyote atakayebainika kuhusika kuwasaidia wasafirisha unga atafukuzwa kazi na ambaye atafanya juhudi ya kuwakamata wasafirishaji hao atapewa zawadi.”

“Kuna watu wanadhani tunafanya mzaha katika jambo hili. Jana baada ya mimi kuondoka usiku wa saa 2:30 huyu (kijana aliyekamatwa) akaingia na mzigo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza kuwa alikamatwa na kete 86 za dawa aina ya heroini na misokoto 34 ya bangi aliyokuwa akiisafirisha kwenda Italia kupitia Zurich.

Aliiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwatunuku wafanyakazi waliofanikisha kukamatwa kwa kijana huyo.

Akizungumzia hali ya Uwanja wa JNIA baada ya kufanya ziara juzi, Dk Mwakyembe alisema tatizo halipo kwenye vitendea kazi, bali wafanyakazi wasiokuwa waaminifu.

“Tulikagua ili kujiridhisha kwa vifaa vilivyopo na tumeridhika kuwa kiwanja ni kizuri, hata Shirika la Kimataifa linalokagua viwanja vya ndege limeukubali kuwa uko vizuri katika vifaa kwa hiyo tatizo lipo kwa sisi wenyewe wenye dhamana.

“Ukaguzi huu utaendelea katika viwanja vyote hapa nchini mpaka bandarini na kila tutakayemkamata tutachapisha picha yake,” alisema Dk Mwakyembe.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini huku wengine wawili wakikamatwa Hong Kong wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya mabilioni ya fedha.

Akizungumzia kijana aliyekamatwa, mmoja wa askari ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema: “Tulipewa taarifa za kiitelijensia saa tisa alasiri na raia mwema kuwa kuna mtu anasafiri na atafika uwanjani hapo kuanzia saa moja usiku na anasafiri kwenda Italia.

“Baada ya kupewa taarifa hizo tulijipanga na ilipofika saa 1:49 usiku alifika kijana mmoja, kwa kuwa tulishaelezwa wajihi wake, hatukupata shida, tulimchukua, tukamhoji na tulipompekua tulimkuta na kete 84.”

Kamanda wa Vikosi vya Uwanja wa Ndege, Deusdedit Kato akizungumzia tukio hilo alisema: “Alikuwa kwenye ukaguzi wa kawaida akiwa kwenye mstari na ilipofika zamu yake aliamriwa akae pembeni akafanyiwa upekuzi.

Alisema Mtanzania anatumia muda mwingi kukaa Italia na kwamba polisi wanaendelea kumfanyia mahojiano ili kujua alikozitoa na mhusika anayempelekea huko.

Alisema dawa hizo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa ili zifahamike ni za aina gani na anatarajiwa kufikishwa Mahakama ya Kisutu kati ya leo na Jumatatu kutegemea kukamilika kwa upepelezi.

FAMILIA YALAANI KUTOLEWA KWA SHEIKH PONDA HOSPITALI


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kulia), ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za uchochezi,  akitolewa katika taasisi ya mifupa MOI, kuelekea katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam majira ya asubuhi leo. (Na Mpiga Picha Wetu)

DAR ES SALAAM, Tanzania

Kwa upande wao familia ya Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo kilichofanywa na serikali cha kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa anaendelea kupata matibabu.

Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na hali hiyo kama familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa salama.

“Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui kwanini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzonui tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa tunaachia hili walizungumzie wao.”alisema Is-haq.


Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa viongozi wa jumuiya na taasisi za kiislamu jana walikuwa katika kikao kizito cha kujadili hatua hiyo ya kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu na kwamba leo watakutana na waandishi wa habari kuelezea msimamo wao.

SHEIKH PONDA APELEKWA GEREZANI SEGEREA


Wakili wa Sheikh Ponda

DAR ES SALAAM, Tanzania

Wakili wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Nassor Jumaa, amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Ponda aliyekuwa  amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu(MOI)  alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumwamishia katika gereza la Segerea.

Wakili Jumaa alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani hakimu Hellen Riwa juzi muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea shitaka Ponda, hakimu Liwa alitoa amri ya Ponda aendelee kukaa chini ya ulinzi lakini cha kushangaza leo,wanausalama wamemtoa wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kwa kweli kitendo hicho kimenisikitisha na kunishitua sana ….ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni’alisema wakili Jumaa.

Agosti 14 mwaka huu, saa kumi jioni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamia katika wodi hiyo ya MOI na wakili wa serikali Tumaini Kweka alimsomea shitaka Ponda ambaye anakabiliwa na kesi hiyo ya Jinai Na.144 ya mwaka huu.
 
CHANZO:HABARI MSETO BLOG

Thursday, August 15, 2013

Ulaya wanavyomuandika Sheikh Ponda


IMG-20130814-WA0001
Nchini Uingereza gazeti la Daily Mail linalotoka kila siku limeandika kwamba, Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda Issa, anaweza kuwa mtuhumiwa mkuu wa tukio la wasichana wawili raia wa nchi hiyo waliomwagiwa tindikali hivi karibuni.
Kirstie Trup (18) na Katie Gee (18t), wakazi wa Hampstead, Kaskazini-Magharibi mwa London ambao wanatibiwa hospitali moja nchini humo, walimwagiwa tindikali Agosti 7, mwaka huu huko visiwani Zanzibar, madai makubwa yakiwa ni kuvaa mavazi yasiyoendana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
MAHUBIRI YA PONDA YATAJWA
Pamoja na kupigwa risasi begani huko Morogoro, kwa mujibu wa gazeti hilo lililoingia mtaani Jumatatu iliyopita, pamoja na kutomhusisha moja kwa moja, Shehe Ponda aliwahi kutoa mahubiri Zanzibar ambayo kwa akili ya kawaida ni kama yalichochea wasichana hao kumwagiwa tindikali.
Gazeti hilo liliandika kuwa kuna uwezekano Kikundi cha Uamsho kuhusika huku mahubiri ya Ponda yakihusishwa na utendaji wa kundi hilo, jambo ambalo hata polisi wanalihisi.
Gazeti hilo lilidai kuwa Shehe Ponda alipigwa risasi huko Morogoro huku akiwa anasakwa huko Zanzibar kwa sababu ya mahubiri yaliyosemekana yalikuwa ya kichochezi.
“Alitembelea Zanzibar wiki kadhaa zilizopita na baada ya mahubiri ya chuki aliyoyatoa kwa wafuasi wake akiwataka kuandamana kupinga ukoloni ndipo Kirstie na Katie wakamwagiwa tindikali.
“Tindikali imekuwa ndiyo silaha kubwa Zanzibar ikitumiwa na kundi hilo linalotaka kujitenga katika nchi ya Tanzania na kuongozwa na Sharia,” liliandika Dail Mail la Uingereza.
GAZETI LINGINE
Gazeti lingine la The Telegraphic la nchini humo liliandika: “Shehe Ponda alitumia wiki nzima Zanzibar mwanzoni mwa Agosti akihubiri misikitini akiunga mkono maandamano ‘kama ya Misri’ hadi ‘memba’ wao 10 waliofungwa waachiwe.
“Alikuwa akizunguka akiwaambia vijana wafanye maandamano yasiyokuwa na kikomo kuonesha wao wana nguvu.”
MTANZANIA AISHIYE LONDON AFUNGUKIA HALI ILIVYO
Mtanzania aishiye Jiji la London, Uingereza (jina tunalo) aliliambia Risasi Mchanganyiko juzi kwamba, baadhi ya Waingereza wametokea kumchukia Shehe Ponda baada ya habari yake na picha kuchapishwa kwenye gazeti hilo likimhusisha na tindikali ya wasichana hao waliokuwa wakijitolea kufundisha huko Zanzibar.
“Waingereza wengi wametokea kumchukia Shehe Ponda huo ndiyo ukweli. Wanasema kama Tanzania hawataichukulia ‘siriasi’ ishu hiyo, basi Shehe Ponda siku akitua London, itakula kwake,” alisema Mbongo huyo.
Aliongeza kuwa sera ya Uingereza tangu Mkutano wa Berlin, Ujerumani mwaka 1884/85 wa nchi za Ulaya kuweka maazimio ya kuitawala Afrika, kila nchi ilitakiwa kulinda watu wake hivyo sera ya Uingereza kwa sasa ni kulinda raia wake wa nje na ndani kwa gharama zozote zile.
“Unakumbuka ule Mkutano wa Berlin mwaka elfu moja mia nane na themanini na nne, nchi za Ulaya ziliweka maazimio kuhusu kujilinda na kuingia katika makoloni ya Afrika.
“Uingereza iliamua kuweka sera ya kulinda raia wake wa ndani na nje kwa gharama yoyote ile.

“Ndiyo maana naweza kusema Ponda atachukiwa tu mpaka mwisho. Unajua Waingereza siku zote wanawachukia watu wenye misamamo mikali, watu wanaoweza kufanya lolote bila kujali uhai wa mtu mwingine,” alisema Mtanzania huyo.
WABONGO WAITAKA SERIKALI KUMWONGEZEA ULINZI PONDA

Jijini Dar es Salaam, juzi baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili nje ya wadi aliyolazwa Shehe Ponda, Hospitali ya Muhimbili waliitaka serikali kumwongezea ulinzi kiongozi huyo.

Bakari, mkazi wa Kigogo, Dar alisema: “Tayari magazeti ya Ulaya yameanza kumtuhumu Ponda kwamba alichochea wale Wazungu kumwagiwa tindikali, ni vyema kama serikali ikawa makini naye.
“Wenzetu (Waingereza) wana uwezo mkubwa na zana kibao, wanaweza kutua juu ya paa la hospitali hapa wakamchukua na kumpeleka Uingereza.”
KISA CHA PONDA NA SERIKALI

Licha ya watu kuitaka serikali kumlinda zaidi Shehe Ponda, tayari kiongozi huyo yuko chini ya ulinzi hospitalini alikolazwa.

Inadaiwa kuwa Shehe Ponda akipona atafikishwa mbele ya sheria kujibu tuhuma za uchochezi wakati akihubiri huko Zanzibar hivi karibuni wakati bado akiwa kwenye kifungo cha nje baada ya kuhukumiwa kifungo cha nje miezi kadhaa iliyopita.
Wakati hayo yakiendelea Bongo, huko London wasichana waliomwagiwa tindikali wanaendelea na matibabu katika Hospitali za Chelsea na Westminster ikielezwa kuwa mmoja atawekewa ngozi ya bandia kutokana na kuharibiwa kupita maelezo.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete alilaani vikali kitendo cha kinyama walichofanyiwa wasichana hao kwa maelezo kuwa ni aibu kwa Tanzania.

A Masjid is being set on fire in ‪#‎rabaa‬ ‪#‎Egypt‬,

A Masjid is being set on fire in ‪#‎rabaa‬ ‪#‎Egypt‬, only a few talk about it.

Sky News/BBC News didn't report that.
While the church that got burnt, the whole world talks about it.

BREAKING NEWS: Dr. Abdurrahman Al-Sumait passed away

 just a couple of hours ago, a man who has nearly outdone an entire nation!

Indeed, we belong to Allah, and we shall return to him. Remember the Shaykh in your Doaa.

Tuesday, August 13, 2013

'Uingereza ikitaka uhusiano na Iran isitishe uhasama'


 Abbas Araqchi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema uhusiano wake na Uingereza unaweza kurejeshwa tu kwa sharti la wakuu wa London kusitisha uhasama wao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Akizungumza leo mjini Tehran katika kikao cha kila wiki na waandishi habari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Sayyed Abbas Araqchi amesema tayari bunge la Iran lilikuwa limeshapunguza kiwango cha uhusiano wa Tehran na London hadi balozi mdogo kabla ya Uingereza kuchukua uamuzi wa upande moja wa kukata kabisa uhusiano baina ya nchi hizi mbili . Kuhusiana na hali nchini Iraq, Araqchi ameelezea masikitiko yake kutokana na hujuma za kigaidi nchini humo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Sikukuu ya Idul Fitr. Amesema hujuma hizo ziko dhidi ya ubinaadamu na Uislamu. Aidha ametoa wito kwa Wairaqi kuwa na subira, kuwa waangalifu na kudumisha umoja wa kitaifa. Kuhusiana na hali ya mambo nchini Misri, Araqchi amesema Jamhuri ya Kiislamu inafuatilia kwa karibu matukio ya nchi hiyo. Amesema wasi wasi uliopo ni kuhusu kuibuka mgawanyika na mpasuko nchini Misri na kutumbukia nchi hiyo katika vita vya ndani jambo ambalo amesema litakuwa ni 'maafa makubwa katika eneo.'. Amesisitiza kuwa migogoro ya Misri, Syria na Lebanon itaufaidisha utawala wa Kizayuni wa Israel tu. Kwa kuzingatia hilo ametoa wito kwa viongozi wa eneo hasa nchini Misri kutumia hekima katika kukabiliana na njama za madola ya kigeni na wahakikishe kuwa umoja wa kitaifa unadumishwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Waathiriwa wa mafuriko Sudan wapata misaada


Waathiriwa wa mafuriko Sudan wapata misaadaUmoja wa Mataifa umeanza kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia walioathiriwa mafuriko nchini Sudan. Mashirika ya misaada ya kibinadamu inayofungamana na Umoja wa Mataifa yameanza zoezi la upelekaji misaada hiyo kwa raia takribani laki moja na nusu waliokumbwa na mafuriko katika viunga vya mji mkuu Khartoum. Kifurushi cha awali cha misaada hiyo ya kibinadamu kinajumuisha chakula na maji safi ya kunywa. Raia hao wameathiriwa na mafuriko hayo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Sudan tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Agosti. Ripoti za utabiri wa hali ya hewa zinaonesha kuwa, mafuriko na mvua kali zitaendelea kunyesha katika siku kadhaa zijazo nchini Sudan na kuathiri idadi kubwa zaidi ya watu. Njia na barabara nyingi za mji wa Khartoum hazipitiki kutokana na kusambaa maji kila mahala huku sehemu kubwa ya mji mkuu huo ikiwa haina huduma ya maji na umeme kutokana na kuharibika miundo mbinu ya huduma hizo

Umasikini wa juu Saudi Arabia


Umasikini wa juu Saudi Arabia  Kiwango cha umasikini nchini Saudi Arabia kiko juu zaidi ya nchi za Lebanon, Jordan na Palestina. Hayo yamethibitishwa na mtaalamu mmoja wa masuala ya kiuchumi alipokuwa akizungumzia hali mbaya ya uchumi nchini Saudia na kusisitiza kuwa, kiwango cha umasikini katika nchi hiyo ya Kiarabu ni cha hali ya juu ukilinganisha na nchi za Lebanon, Jordan, Palestina, Tunisia na Syria. Aidha mtaalamu huyo wa masuala ya kiuchumi amesema kuwa, kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo nacho kiko juu zaidi ya nchi za Afrika. Mtaalamu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kiwango hicho cha umasikini kilichopo nchini humo kinazidi hata zile nchi zinazopata misaada kutoka kwa Saudia yenyewe na kusisitiza kuwa, ripoti hiyo ipo pia hata katika mtandao wa benki ya dunia. Ameenda mbali zaidi na kusema kuwa, asilimia 99 ya wafanyakazi wengi wa serikali nchini humo wakiwemo maafisa wa jeshi na vyombo vya usalama, wanadaiwa na mabenki ya Saudia. Hii ni katika hali ambayo, Saudia ni mzalishaji mkubwa wa mafuta huku asilimia 70 ya utajiri wote wa nchi hiyo, ukielekea kwenye mifuko ya familia ya kifalme.

Sunday, August 11, 2013

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu Sheikh Ponda

Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, akiwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, akiwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.



Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wizara ya Mambo ya Ndani.
Jeshi la Polisi Tanzania.
Dar es Salaam
Agosti 10, 2013
1. Mnamo tarehe 10, Agosti, 2013, majira ya saa 8 mchana, maeneo ya shule ya msingi ya kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro kulifanyika kongamano la Baraza la Eid lililoandaliwa na Umoja wa wahadhiri mkoani Morogoro,
Dakika chache kabla ya kongamano hilo kumalizika alifika Shekhe Ponda issa Ponda alizungumza kwa muda mfupi.
2. Kongamano hilo ambalo lilifungwa majira ya saa 12:05 jioni,
Ambapo watu walianza kutawanyika, baadhi yao wakiwa wamezingira gari dogo alilokuwa amepanda Shekhe Ponda baada ya kutoka katika eneo hilo, askari wa Jeshi la Polisi walilizuia gari hilo kwa mbele kwa nia ya kutaka kumkamata Shekhe Ponda ambaye anatuhumiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi sehemu mbalimbali hapa nchini yenye mlengo wa kusababisha uvunjifu wa amani.

3. Baada ya askari kutaka kumkamata, wafuasi wake walizuia ukamataji huo kwa kuwarushia mawe askari wa Jeshi la Polisi, kufuatia na purukushani hizo askari walipiga risasi hewani kama onyo la kuwatawanya.
4. Katika vurugu hizo, wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha mtuhumiwa, hivi sasa imethibitishwa kuwa Shekhe Ponda yupo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akitibiwa majeraha katika bega la mkono wa kulia linalodaiwa alilipata katika purukushani hizo.
5. Kufuatia tukio hilo timu inayoshirikisha wajumbe toka jukwaa la haki jinai ikiongozwa na CP Issaya Mngulu imeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
SSP Advera Senso
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, akiwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, akiwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kauli ya Mtatiro juu ya Sheikh Ponda



MTATIRO

UNYAMA ALIOFANYIWA SHEIKH PONDA HAUKUBALIKI, ULAANIWE KWA NGUVU ZOTE.
Muda si mrefu nimetoka kuongea na shuhuda mmoja aliyekuwepo Morogoro. Ni kweli kuwa Sheikh PONDA amejeruhiwa vibaya kwa RISASI.
Huu ni mwendelezo wa matukio ya kuwawinda viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, waandishi wa habari na wanaharakati ambao serikali inaamini ni “watu hatari”.
Hivi karibuni, taarifa za ndani za serikali zimekuwa zikimuonesha Sheikh Ponda kama “mtu hatari kwa usalama wa taifa”, huu ni upuuzi na ujinga mkuu ambao utatupeleka pabaya.
Ikiwa kuna mtu ni hatari sana kwa taifa, na serikali ina ushahidi, kwa nini isimfungulie mashtaka mtu huyo na ipeleke ushahidi huo mahakamani ili mahakama ipime na kuamua au la!
Serikali inayotumia “approach” (mbinu) ya kushambulia, kujeruhi kwa nia ya kuwaua watu wenye msimamo tofauti na serikali hiyo, hii inakuwa “serikali hatari, ya kijinga, dhaifu na iliyoshindwa kuongoza”, serikali ya namna hii “is more dangerous to the peace of the nation than the dangerous persons themselves” (serikali ya namna hii ni serikali hatari mno kwa amani ya taifa kuliko watu inaowadhania kuwa hatari”.
Mimi nachojua, Sheikh Ponda ni mwanaharakati wa kiislamu anayebeba matumaini, hoja na visheni ya waislamu walio wengi. Kwa upande mwingine serikali ya CCM inamuona Sheikh PONDA kama mtu hatari kwa sababu hoja na visheni zake vikifanikiwa vitawatoa waislamu chini ya BAKWATA ambayo inatumiwa na serikali ya CCM kama nyenzo ya kuwadhibiti waislamu katika masuala yao ya msingi na hata baadhi ya haki zao muhimu za kiimani.
Serikali yoyote ya kipuuzi na iliyokufa “a failed state” haifikiri namna ya kutafakari hoja zinazokinzana na serikali na kuzitafutia ufumbuzi mezani. Hufikiri kutumia nguvu, kuwatisha watoa hoja husika na hata kuwaua pale nafasi inapopatikana, ilimradi udhibiti “sensorship” uendelee.
Serikali mfu kama ya CCM huwasha kiberiti yenyewe na baadaye huhaha kuzima moto ikiwalaumu watu wengine kwa matatizo yaliyoanzishwa na serikali yenyewe.
Ikiwa viongozi tutachekelea unyama huu na kuacha fulani atambuliwe kama “mtu hatari sana” ATI kwa sababu tu yeye ni dini fulani, ni kweli mhusika atashughulikiwa ipasavyo, atateswa tutachekelea, ataumizwa tutasheherekea na atauawa tutapiga nderemo na vifijo.
Serikali mfu haitaishia hapo, ikimaliza kumshughulikia yeye kwa dini yake itahamia kwako, itakuita “mtu hatari sana” kwa sababu ya chama chako, kwa sababu ya uanaharakati wako, kwa sababu ya uandishi wako na kwa sababu ya msimamo na mtizamo wako ambao unapingana na serikali. Nani atabaki salama?
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, “ukinywa damu ya mtu, utaendelea kunywa tu”. Nami nasema, tukichekelea na kukubali propaganda za CCM kuwa Sheikh Ponda ni mtu hatari sana, akishamalizwa watahamia kwetu(kwangu na kwako), mimi na wewe tutapewa “uhatari” na tutasakwa kwa mtutu wa bunduki tuuawe haraka ili taifa libaki kuwa salama.
Serikali ya CCM iache mbinu hizi ambazo tulishazijua. Serikali ikatatue tatizo la msingi la MZOZO WA MIONGO KADHAA KATI YAKE NA WAISLAMU. CCM iwaache waislamu watafute uongozi wao huru kabisa, wanaouamini. Kufikiri ATI maoni ya waislamu yataendelea kusimamiwa, kuratibiwa na kuongozwa na BAKWATA ni kupoteza muda na kijidanganya. Mbona sisi wakristu tuna taasisi zetu muhimu na imara za kidini na tunaziamini? Kwa nini serikali ya CCM inaendelea kuwashika waislamu na kuwadhibiti kwa kuitumia taasisi ambayo waislamu hawaiamini?
Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, pamekuwa na marais wawili ambao ni waumini wa dini ya kiislamu, Mzee Mwinyi na sasa Mhe. Kikwete, hawa ni waislamu kabisa, ina maana hawajui malalamiko ya waislamu ya miaka nenda rudi? Kama Kikwete na wenzie walichoshwa na mauaji yaliyokuwa yanaendelea Zanzibar na wakaamua kuwaacha wazanzibari waamue hatima yao na Leo imeundwa SUK. Kina Kikwete haohao wanashindwaje kusema matatizo ya waislamu sasa basi na wakawaachia waislamu huru waamue hatima yao, wawe na vyombo wanavyoviamini visimamie maslahi yao. Mwinyi na sasa Kikwete siyo waislamu? CCM ina maslahi gani BAKWATA?
Mtizamo wangu pia ni kwamba, waislamu wanaweza kuwa wanamalizana wao kwa wao bila kujua.
Pale Marekani kulikuwa na tatizo la msingi kwa wamarekani wengi wa kipato cha chini, huduma za afya zilikuwa kuzungumkuti. Sehemu kubwa ya waathirika wa jambo hili walikuwa wamarekani weusi. Marais wote wazungu waliopita hawakuwahi kufikiri kulitatua, alipopata nafasi Obama akalibainisha Suala la afya kwa wamarekani wa kipato cha chini kama tatizo la msingi linalohitaji utatuzi wa haraka. Obama akatengeneza muswada wa bima ya afya, akambana hadi ukawa sheria, Leo wamarekani wa kipato cha chini ambao wengi ni weusi wanafaidika na mpango huo. Obama alipigwa vijembe kuwa analeta muswada wa kuwapendelea watu weusi lakini aliwapuuza wapinzani wake, alijua anafanya jambo ambalo litaondoa mgawanyiko na ukosefu wa haki muhimu ambalo lingeisumbua Marekani ya baadaye.
Hapa kwetu tuna marais wanaonea haya dini zao na wanashindwa kutatua matatizo ya msingi ya kundi ambalo wameliishi na kuonja adha ya kero zao. Kuwaacha waislamu wajichagulie vyombo huru vya kujiongoza ni kuongeza na kupanua wigo wa demokrasia na uhuru muhimu kwa watanzania wote, hili halitakuwa na faida kwa waislamu peke yao, lina faida kwa nchi nzima. Ni bora rais uitwe mdini kwa kuondoa udhibiti wa chama chako kwa taasisi ya kidini na kuiacha huru kuliko kuacha mifarakano na malalamiko ya kundi linalodhaniwa linaonewa kwa miongo kadhaa yaendelee.
Mimi nadhani waislamu wana matatizo ya msingi kati yao, panahitajika viongozi imara wanaoliona hilo. Ikiwa yataachwa au kushughulikiwa kwa mtindo huu wa kuvizia na kupiga RISASI wale wanaotetea maslahi halisi ya waislamu, hayatakwisha.
Ikiwa atauawa Ponda mmoja eti kwa sababu anadhaniwa kuwa “mtu hatari”, in the next morning watazaliwa Ponda wengine hatari zaidi wapatao 1000. Uhuru wa Dokta hauzimwi kwa RISASI.
Sote bila kujali itikadi zetu za kidini, kisiasa na kimtizamo, TULAANI KWA NGUVU UNYAMA ALIOFANYIWA SHEIKH PONDA.
Julius Mtatiro,
+255717536759.
Maoni haya ni yangu binafsi, yasihusishwe na chama changu wala nafasi yangu ya uongozi ndani ya chama.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIOJIRI KATIKA KONGAMANO LA SHEIKH PONDA JANA MOROGORO

 Kutambulishwa jukwaani Shekh Ponda.
 Askari wa FFU wakijisongeza kati kati ya uwanja mara baada ya muda wa kongamano kumalizika.
 Kikosi cha FFU uwanjani
 Shekh Ponda akikaribishwa kwenye jukwaa kuu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , mjini Morogoro
 Shekh Ponda akisalimiana na Mhadhiri wa Mihadhara nchini, Ustaadhi Abubakari
 Shekh Ponda akisisistiza jambo mbele ya waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Kongamano , Augosti 10, mwaka huu mjini Morogoro
 Shekh Ponda akiteta jambo na baadhi ya Viongozi wa umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoa wa Morogoro
 Shekhe Ponda akiwa meza kuu kwenye kongamano hilo
 Shekhe Ponda akiwa amezingirwa na waumini
 Umati wa waumini wa Kiislamu wakimsikiliza Shekh Pond
Waumini wa Dini ya Kiislamu wa mjini Morogoro wakimsikiliza Shekh Ponda
Waumini wa Kiislamu wakitawanyika uwanjani baada ya muda wa kongamano kufikia tamati,