Mahakama ya Misri imeamuri dikteta Hosni Mubarak kuachiliwa huru
baada ya mahakama hiyo kusema kuwa hakupatwa na hatia katika kesi
iliyokuwa imebakia ya ubadhilifu. Kwa mujibu wa wakili wake na duru za
mahakama za Misri, leo Jumatatu korti imeamuru Mubarak aachiliwe huru
katika kesi ambayo yeye na watoto wake wawili Alaa na Gamal walikuwa
wakituhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma. Taarifa hiyo inasema
kwamba, Mubarak anaweza kuachiliwa huru wiki hii, lakini watoto wake
wawili wataendelea kushikiliwa. Huko nyuma pia iliamriwa kwamba dikteta
huyo wa Misri aachiliwe huru katika kesi nyingine mbili ambapo
alishitakiwa kuhusika katika mauaji ya waandamaji wakati wa harakati za
maandamano ya mwaka 2011 ambayo yalimuaondoa madarakani na pia
kujilimbikizia mali kinyume cha sheria. Wamisri wengi wanaamini kuwa
Mubarak aliyekuwa kibaraka mkubwa wa Marekani na Israel wakati wa
utawala wake anapaswa kuhukumiwa kifo kutokana na kuwaua waandamanaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment