Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, August 13, 2013

'Uingereza ikitaka uhusiano na Iran isitishe uhasama'


 Abbas Araqchi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema uhusiano wake na Uingereza unaweza kurejeshwa tu kwa sharti la wakuu wa London kusitisha uhasama wao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Akizungumza leo mjini Tehran katika kikao cha kila wiki na waandishi habari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Sayyed Abbas Araqchi amesema tayari bunge la Iran lilikuwa limeshapunguza kiwango cha uhusiano wa Tehran na London hadi balozi mdogo kabla ya Uingereza kuchukua uamuzi wa upande moja wa kukata kabisa uhusiano baina ya nchi hizi mbili . Kuhusiana na hali nchini Iraq, Araqchi ameelezea masikitiko yake kutokana na hujuma za kigaidi nchini humo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Sikukuu ya Idul Fitr. Amesema hujuma hizo ziko dhidi ya ubinaadamu na Uislamu. Aidha ametoa wito kwa Wairaqi kuwa na subira, kuwa waangalifu na kudumisha umoja wa kitaifa. Kuhusiana na hali ya mambo nchini Misri, Araqchi amesema Jamhuri ya Kiislamu inafuatilia kwa karibu matukio ya nchi hiyo. Amesema wasi wasi uliopo ni kuhusu kuibuka mgawanyika na mpasuko nchini Misri na kutumbukia nchi hiyo katika vita vya ndani jambo ambalo amesema litakuwa ni 'maafa makubwa katika eneo.'. Amesisitiza kuwa migogoro ya Misri, Syria na Lebanon itaufaidisha utawala wa Kizayuni wa Israel tu. Kwa kuzingatia hilo ametoa wito kwa viongozi wa eneo hasa nchini Misri kutumia hekima katika kukabiliana na njama za madola ya kigeni na wahakikishe kuwa umoja wa kitaifa unadumishwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment