Nabil Fahmy, Waziri wa Mambo ya Nje
wa serikali ya mpito ya Misri iliyowekwa madarakani na jeshi ametetea
ukandamizaji na umwagaji mkubwa wa damu uliofanywa hivi karibuni na
jeshi dhidi ya wafuasi wa Muhammad Morsi, rais wa nchi hiyo
aliyeng’olewa madarakani na jeshi. Akizungumza na waandishi wa habari
mjini Cairo Fahmy amesema serikali ya mpito imeonyesha uvumilivu katika
kukabiliana na waandamanaji na itaendelea kufanya hivyo. Matamshi hayo
yametolewa huku Muungano Dhidi ya Mapinduzi unaojumuisha makundi kadhaa
ikiwemo harakati ya Ikhwanul Muslimin ukijipanga kufanya maandamano
mapya mjini Cairo. Zaidi ya watu 800 wameuawa na maelfu kadhaa
kujeruhiwa katika ukandamizaji uliofanywa na jeshi na polisi ya Misri
dhidi ya maandamano yaliyofanyika siku ya Jumatano na Ijumaa katika miji
kadhaa ya Misri. Wakati huohuo jumuiya kadhaa za kutetea haki za
binadamu ndani na nje ya Misri zinajiandaa kuchukua hatua ya kuwasilisha
mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC dhidi ya Jenerali
Abdulfatah al Sisi pamoja na maafisa wengine wa kijeshi na wa kiraia wa
serikali ya mpito kwa kuhusika na mauaji ya hivi karibuni ya raia.
Jumuiya hizo zimeeleza kuwa zinakusanya nyaraka na ushahidi ili
kumfikisha katika Mahakama ya ICC Waziri wa Ulinzi al Sisi, Waziri wa
Mambo ya Ndani Muhammad Ibrahim na maafisa wengine kadhaa wa jeshi…/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment