Pichani
juu ni taswira za ajali ya basi iliyouwa watu 41 na kujeruhi 33 katika
eneo la Ntulele lililo kwenye mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya. Basi
hilo lilikuwa likiwasafirisha zaidi ya abiria 60 kutoka mji mkuu wa
Kenya, Nairobi kuelekea mji wa Homabay uliopo magharibi mwa Kenya
lilikosa mwelekeo na kupinduka mara kadhaa usiku wa kuamkia Alhamisi.
Watu 33 walifariki papo hapo huku wengine 8 wakifariki baadaye
walipokuwa wakipata matibabu hospitalini. Watu wengine 33 waliopata
majeraha mabaya wanaendela kupata matibabu kwenye hospitali tofauti
nchini Kenya. Akituma rambirambi zake kwa familia za marehemu, rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta amewataka madereva kuwa waangalifu na kuongeza kuwa
hatua zitachukuliwa kuhakikisha maisha ya Wakenya hayapotei kwa ajali
za barabarani. (Picha na Nation)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment