Taarifa ya polisi ya Kenya ambayo hadi sasa haijamtia nguvuni mtu aliyemuua msomi huyo wa Kiisalmu, imesema kuwa kundi la al Shabab linaloshirikiana na mtandano wa al Qaida, huenda linapanga kufanya mashambulizi ya kukumbuka kuuliwa msomi huyo.
Mkuu wa polisi ya kaunti ya Mombasa Robert Kitur amesema jeshi la polisi limepata taarifa za kipelelezi kuhusu tishio la shambulizi la kundi la al Shabab katika mji wa Mombasa katika kumbukumbu ya mauaji ya Sheikh Aboud Rogo. Kitur amesema usalama umeimarishwa zaidi katika mji wa Mombasa na kwamba polisi imezuiya maandamano ya kukumbuka tukio la kuuawa Sheikh Rogo.
Waislamu wengi wa Kenya wanaituhumi serikali ya nchi hiyo kwamba ilihusika na mauaji ya Sheikh Aboud Rogo yaliyofanyika Agousti 27 mwaka jana. Vyombo vya usalama vya Kenya hadi sasa havijamkamata mtu au watu waliofanya mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment