Rais mpya wa Mali Ibrahim Boubacar
Keita ametoa wito kwa watu wote nchini humo kushikamana na misingi na
thamani za Kiislamu ili kuleta umoja na maelewano ya kitaifa.
Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo
Bamako kwa mara ya kwanza baada ya ushindi katika uchaguzi wa rais
uliofanyika hivi karibuni, Keita alisema mambo atakayoyapa umuhimu ni
utawala wa kisheria, kuliimarisha jeshi na kupambana na ufisadi.
Keita amesisitiza kuwa yeye atakuwa rais
wa watu wote wa Mali na kwamba sasa hakuna haja tena ya uhasama baina
ya makundi mbali mbali nchini humo. Ibrahim Boubacar Keita ambaye
ataapishwa mwezi ujao wa Septemba amesema hivi sasa Mali inakabiliwa na
changamoto nyingi ambazo zinaweza kutatuliwa tu kwa kutegemea thamani za
Kiislamu na kuvumiliana. Mgogoro wa Mali ulianza tarehe 22 Machi mwaka
huu wakati wanajeshi waasi wakiongozwa na Amadou Sanogo walipofanya
mapinduzi yaliyomng'oa madarakani Rais Amadou Toumani Toure kwa madai
kuwa ameshindwa kuzima uasi kaskazini mwa nchi hiyo. Baada ya hapo waasi
walichukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Hivi sasa baada
ya uchaguzi utulivu umerejea nchini humo.
No comments:
Post a Comment