Abubakar Shekau amekua kiongozi wa Boko Haram tangu mwaka wa 2009. Kundi lake limeendesha mashambulizi ya mabomu na utekaji nyara wa raia. |
Huenda kiongozi wa kundi la Boko
Haram nchini Nigera, Abubakar Shekau aliuawa na maafisa wa usalama
katika ufyatulianaji wa risasi. Duru za kijeshi zinasema huenda Shekau
aliuawa kati ya Julai 25 na Agosti 3.
Shekau alipata majeraha mabaya na kuvukishwa hadi katika mji ulioko mpaka na Cameroon kwa matibabu. Inaaminika alikufa kati ya Julai 25 na Agosti tatu mwaka huu. Waandishi wa habari wamesema hakuna taarifa huru ambazo zimethibitisha kifo cha Shekau.
Maelfu ya raia wameuawa tangu Boko Haram kaunza maasi mwaka 2009. Abubakar Shekau alichukua uwongozi wa wapiganaji hao wa kiisilamu baada ya kifo cha mwanzilishi wa Boko Haram, Muhammad Yusuf aliyefariki dunia wakati akiwa kizuizini.
Kundi hilo limeendesha mashambulizi mabaya na ya kikatili wakati wa uwongozi wa Shekau. Boko Haram wamekuwa wakishinikiza kuunda taifa la Kiisilamu nchini Nigeria.
Hapo mwezi Mei mwaka huu Rais Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu Kaskaizni mwa Nigeria ambapo pia alituma jeshi kuendesha operesheni dhidi ya wapiganaji hao.
Chanzo : BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment