Safari za kimataifa za ndege
zimeanza tena leo asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta mjini
Nairobi, Kenya baada ya eneo kubwa la uwanja huo kuteketezwa na moto
siku ya Jumatano alfajiri.
Uwanja huo ulifungwa kwa muda jana na ndege zililazimika kutua Mombasa na katika nchi jirani.
Mkuu wa usalama katika uwanja wa Jomo
Kenyatta Bw. Eric Kiraithe amesema wasafiri wa kimataifa watatumia eneo
la wasafiri wa ndani ya nchi baada ya eneo la wasafiri wa kimataifa
kuteketezwa kabisa katika moto wa jana. Taarifa zinasema zaidi ya
wasafiri 16,000 ambao hupita katika uwanja huo kila siku waliathiriwa
vibaya na mkasa huo wa moto.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana
alifika katika uwanja huo wa ndege na kutoa taarifa kupitia msemaji wake
Manoah Esipisu na kusema sababu za moto huo zinachunguzwa hivyo watu
wajiepushe na uvumi. Alisema hatua zinachukuliwa kuhakikisha shughuli za
uwanja huo zinarejea katika hali ya kawaida.
No comments:
Post a Comment