skip to main |
skip to sidebar
Umasikini wa juu Saudi Arabia
Kiwango cha umasikini nchini Saudi Arabia kiko juu zaidi ya nchi
za Lebanon, Jordan na Palestina. Hayo yamethibitishwa na mtaalamu mmoja
wa masuala ya kiuchumi alipokuwa akizungumzia hali mbaya ya uchumi
nchini Saudia na kusisitiza kuwa, kiwango cha umasikini katika nchi hiyo
ya Kiarabu ni cha hali ya juu ukilinganisha na nchi za Lebanon, Jordan,
Palestina, Tunisia na Syria. Aidha mtaalamu huyo wa masuala ya kiuchumi
amesema kuwa, kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo nacho kiko juu
zaidi ya nchi za Afrika. Mtaalamu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe
amesema kiwango hicho cha umasikini kilichopo nchini humo kinazidi hata
zile nchi zinazopata misaada kutoka kwa Saudia yenyewe na kusisitiza
kuwa, ripoti hiyo ipo pia hata katika mtandao wa benki ya dunia. Ameenda
mbali zaidi na kusema kuwa, asilimia 99 ya wafanyakazi wengi wa
serikali nchini humo wakiwemo maafisa wa jeshi na vyombo vya usalama,
wanadaiwa na mabenki ya Saudia. Hii ni katika hali ambayo, Saudia ni
mzalishaji mkubwa wa mafuta huku asilimia 70 ya utajiri wote wa nchi
hiyo, ukielekea kwenye mifuko ya familia ya kifalme.
No comments:
Post a Comment