Wanawake wawili raia wa Uingereza wamemwagiwa tindikali usoni Jumatano usiku mjini Zanzibar, Tanzania.
Imearifiwa kuwa wanawake hao wenye umri
wa miaka 18 walishambuliwa na watu wasiojulikana walipokuwa wakitembea
katika mitaa ya Stone Town. Duru zinaarifu kuwa washambuliaji walikuwa
wanaume wawili waliopanda vespa.
Naibu Mkuu wa Polisi Zanzibar Mkadam
Khamis amenukuliwa na AFP akisema, polisi wanawasaka waliotekeleza
hujuma hiyo. Amesema sababu ya kushambuliwa raia hao wawili wa Uingereza
haijabainika.
Katika siku za hivi karibuni kumeongezeka vitendo vya kuwamwagia watu tindikali nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment