skip to main |
skip to sidebar
Israel yaruhusu kutumiwa silaha za kemikali
Waziri wa Afya wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa
Palestina inayoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina
Hamas amelaani vikali hatua ya Mahakama Kuu ya utawala wa Kizayuni wa
Israel ya kuruhusu utumiwaji gesi ya kemikali yenye mada za fosforasi
nyeupe. Mufid al Mukhlalati amesema kuwa, hatua ya mahakama hiyo
kuruhusu utumiwaji wa gesi hizo za kemikali zenye mada za fosforasi
nyeupe, kunalipa nguvu jeshi la utawala huu kutengeneza silaha hatari za
kemikali zitakazotumiwa dhidi ya wananchi wa Palestina. Tarehe 9 Julai
mwaka huu, Mahakama Kuu ya Israel ilitangaza kuwa, utumiwaji wa gesi
hiyo ya kemikali ni ruhusa kabisa. Waziri wa Afya wa Palestina amesema
kuwa, hivi sasa mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yanafanya
juhudi za kuzuia jinai zinazofanyika ulimwenguni kote, lakini vyombo vya
sheria vya utawala wa Israel vinapuuzia sheria za kimataifa kwa
kuruhusu utumiwaji wa gesi za kemikali zenye mada za fosforasi nyeupe
No comments:
Post a Comment