Maelfu
ya watu walifika hospitali binafsi ya uzazi kwenye jiji la Kotaworo
eneo la Bida, iliyopo jimbo la Niger juzi Jumapili, kwa lengo la kwenda
kumshuhudia mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa rozari ya Kiislamu
(Tasbihi) shingoni mwake.
Inaelezwa
kwamba mama wa mtoto huyo ambaye ana miaka ya kati, Adijat, alikimbizwa
hospitali karibu na nyumbani kwa Pa Mohammed Bello Masaba, mda wa saa 8
mchana na baada ya pilika za uzazi alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.
Kwa
mujibu wa mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa
Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema, “Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi shingoni mwake, na wakati wa uzazi mtoto alizaliwa akiwa na Rozari nyeusi.” Alisema Shasha.
“Ila nilishangaa baada ya muda rozari hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe huku kukiwa na watu wengine wamezunguka.”
“Mara
baada ya habari hiyo kusambaa mjini, maelfu ya watu walifika kwenye
hospitali hiyo ya uzazi huku wakisema “Allahu Akibar; Allahu Akibar
(Mungu ni Mkubwa) huku wakifika na kumgusa mtoto huyo.”
Juhudi
za kumpata Baba wa mtoto huyo aitwaye Isah, ambaye anatokea eneo la
Loma ndani ya Jimbo la Kwara State zilishindikana baada ya kukataa
kuongea na mtoa habari.
Mwanachuo mmoja wa Kiislamu, Malam Idiris Ndajiwo alisema, kuzaliwa kwa mtoto huyo akiwa na rozari
“inaonyesha
ukuu wa Allah. Kuzaliwa kwa mtoto huyu leo, kwenye mji huu na eneo hili
(Kutaworo) ni kitu kikubwa kwa Waislamu. Hii hakika inakuja kuonyesha
kwamba Allah ndiye mwenye kupanga kwa lolote kutokea kwa yeyote kwenye
ulimwengu huu.”
No comments:
Post a Comment