skip to main |
skip to sidebar
Uvamizi wa Wazayuni al-Aqswa walaaniwa
Serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina imelaani
uvamizi wa mara kwa mara wa Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Masuala ya Quds katika Wizara ya
Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa wa Serikali ya Palestina inayoongozwa
na Waziri Mkuu Ismail Hania imebainisha kwamba, utawala wa Kizayuni wa
Israel umeendelea kufanya uvamizi wa mara kwa mara katika mji wa Quds na
dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa. Taarifa hiyo imebainisha
kwamba, mipango na njama zote za adui Mzayuni zitashindwa kwani eneo
hilo takatifu ni mali ya Waislamu wote ulimwengu. Aidha taarifa hiyo
imeongeza kuwa, Waislamu kote ulimwenguni wanapaswa kuuhami msikiti wa
al-Aqswa na kutouruhusu utawala wa Kizayunio wa Israel kufikia malengo
yake haramu.
No comments:
Post a Comment