Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mkono wa pole kwa
serikali na wananchi wa Uhispania kutokana na ajali ya treni iliyotokea
hivi karibuni nchini humo na kupelekea watu wasiopungua 80 kufariki
dunia na wengine wasiopungua 140 kujeruhiwa 20, kati ya hali zao
mahututi. Sayyid Abbas Araqchi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje
wa Iran amesema kuwa, ajali hiyo ya treni imeleta majonzi ulimwenguni
kote, hivyo serikali pamoja na wananchi wa Iran wanaungana na wenzao wa
Uhispania kwenye kipindi hiki kigumu cha huzuni na maombelezo. Ajali
hiyo ilitokea siku ya Jumatano, pale treni hiyo kutembea mwendo wa kasi
katika kona na kusababisha mabehewa 13 kuondoka kwenye reli, na manne
kupinduka kabisa. Taarifa zinasema kuwa, dereva wa treni hiyo
anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi, ingawa alishatoa tahadhari
ya kuanguka kwa treni hiyo, baada ya kushindwa kuidhibiti treni hiyo
iliyokuwa kwenye mwendo wa kasi kubwa. Treni hiyo ilikuwa ikitoka
Madrid na kuelekea El Ferrol, na kupata ajali katika mji wa Santiago de
Compestela, ulioko katika mkoa wa Galicia. Hii inahesabiwa kuwa ajali
mbaya zaidi ya treni kutokea nchini humo tokea mwaka 1972.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment