Idadi kubwa ya wahamiaji wanaoelekea kusini mwa Afrika wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kiafya.
Hayo yamebainika katika utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM kwa ushirikiano na taasisi ya masuala ya afya kusini na mashariki mwa Afrika, PHAMESA. Utafiti huo unaonyesha hatari za kiafya zinazowakabili raia wanaohama makwao kutoka nchi za Maziwa makuu, Afrika Mashariki na hata pembe ya Afrika kuelekea Kusini mwa Afrika.
Matokeo ya awali ya utafiti huo yamewasilishwa kwenye mkutano wa pili wa mawaziri wa nchi za kusini mwa Afrika kuhusu mashauriano juu ya uhamiaji huko Maputo, Msumbiji.
Utafiti huo unaonyesha wahamiaji hao hukabiliwa na hatari kubwa za kiafya kutokana na mbinu za usafiri wanazotumia na wanapokamatwa hufungwa katika vizuizi vyenye suhula duni ambao wengi huambukizwa magonjwa hatari. Idadi kubwa ya wakimbizi hao hupoteza maisha njiani kutokana na kusafirishwa ndani ya kontena za mizigo zisizo na madirisha. Aidha wengi hukosa maji na chakula huku wanawake wakinajisiwa. Wakimbizi kutoka nchi kama Ethiopia na Somalia hulipa hadi dola elfu tano kwa safari iliyojaa hatari ya kufika Afrika Kusini nchi ambayo wanaoiona yenye fursa nzuri za kimaisha.

No comments:
Post a Comment