Watu wasiopungua 11 wameuawa katika siku mbili za machafuko kati
ya wafuasi na wapinzani wa Muhammad Morsi, rais aliyepinduliwa na jeshi
nchini humo. Watu waliokuwa na silaha waliwavamia wafuasi wa Morsi
waliokuwa wameketi chini karibu na Chuo Kikuu cha Cairo hapo jana na
kuwauwa wawili kwa riasi.
Kuuliwa wafuasi hao wawili wa Morsi hapo jana kumeifanya idadi ya watu waliouawa huko Misri katika siku za Jumatatu na Jumanne kufikia 11.
Wakati huo huo watu wa familia ya Morsi wamesema watamchukulia hatua za kisheria Abdul Fatah as Sisi na jeshi lake kwa hatua yao ya kumuweka korokoroni Muhammad Morsi.
Itakumbukwa pia kuwa, juzi Jumatatu Rais Adly Mansour wa serikali ya mpito ya Misri alitoa wito wa kufikiwa mapatano ya kitaifa akisema kuwa ni muhimu kwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na kuna udharura wa kuupa umuhimu mustakbali wa wananchi.

No comments:
Post a Comment