Maandamano
hayo yalikuwa ya kupinga uingiliaji kati na uchokozi ulio wa wazi wa
Serikali ya Ethiopia dhidi ya Ardhi ya Kislaam ya Somalia.
Kwenye
Barabara ya mji wa Buula Barde walionekana mamia ya Wananchi waliokuwa
wakipita kweye Barabara hizo huko wakitamka maneno dhidi ya Adui asilia
ya Uvamizi wa Ethiopia aliyovishwa vazi la AMISOM.
Wazee
wa koo wa Mkoa wa Hiraan,wanataaluma,walizungumza kwenye Maandamano
hayo na kusema kuwa watakuwa tayari kuingia vita itakayochukua muda
mrefu dhidi ya wanajeshi wa Ethiopia ili kuilinda Dini na Ardhi
yao,waandamanaji wote hao waliokuwa wakipinga Wanajeshi wa Ethiopia kwa
ujumla wamekubaliana kuwa Uingiliaji wa Ethiopia uliokuja na sura mpya
hautoweza kuathiri chochote harakati iliyokuwa ikiendelea dhidi ya
Maadui wa Kigeni walioivamia Rdhi ya Kislaam ya Somalia.
No comments:
Post a Comment