Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa
Ulaya wamepitisha mpango wa kupelekwa wanajeshi 500 wa umoja huo huko
Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa lengo la kusaidiana na vikosi vya nchi za
Kiafrika na vile vya Ufaransa katika kuleta amani nchini humo.
Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa,
lengo la kutumwa wanajeshi hao ni kutekelekeleza operesheni za
kukomesha machafuko na mauaji dhidi ya wananchi wa nchi hiyo na hasa
Waislamu ambao wamekuwa wakilengwa na mashambulio ya wanamgambo wa
Kikristo wa Anti Balaka. Siku ya Jumapili iliyopita, Shirika la
Kutetea Haki za Bindamu la Human Rights Watch HRW lilitahadharisha kuwa, machafuko yanaondelea kushuhudiwa nchini humo yatasababisha Waislamu wote kuwa wakimbizi. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, karibu watu milioni mbili wanahitaji misaada ya kibinadamu nchini humo.

No comments:
Post a Comment