Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, February 11, 2014

Jeshi la Syria lasisitiza kupambana na magaidi


Jeshi la Syria lasisitiza kupambana na magaidi
Mkuu wa vikosi vya  ulinzi na usalama nchini Syria amesisitiza juu ya kutiwa mbaroni wale wote waliohusika na mauaji ya halaiki ya wananchi wasiopungua 71 wa Syria hapo jana. Mkuu wa majeshi ya Syria ameongeza kuwa, serikali ya Damascus inafanya juhudi za kutatua mateso yanayowakabili  wananchi zinazosababishwa na  njama za baadhi ya mataifa ya nchi za Magharibi na vibaraka wao walioko katika eneo la Mashariki ya Kati. Mkuu wa Majeshi ya Syria amesisitiza kuwa, jeshi la nchi hiyo litaendelea kupambana kikamilifu na kuhakikisha kwamba watenda jinai wa kundi la al Nusra wanahilikishwa kikamilifu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, magaidi walioko nchini Syria, baada ya kukiteka kijiji cha Maan kilichoko Hamah magharibi mwa Syria waliwauwa kwa halaiki watu 71 wakiwemo wanajeshi 50 wa serikali ya Syria. Mauaji hayo yanatokea katika hail ambayo, leo hii inaanza duru ya pili ya mazungumzo kati ya ujumbe wa serikali ya Syria na wapinzani huko Uswisi.

No comments:

Post a Comment