Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, February 11, 2014

Ikhwanul Muslimin ya Misri yakadhibisha kuunda jeshi

Ikhwanul Muslimin ya Misri yakadhibisha kuunda jeshi
Kiongozi mmoja mwandamizi wa harakati ya Ikhwanul Muslimiin ya Misri amesema kuwa, harakati za kundi hilo zitaendelea kuendeshwa kwa njia za amani na kusisitiza kwamba kundi hilo halina mpango kabisa wa kuanzisha tawi la kijeshi.
Muhammad Ali Beshr amekadhibisha vikali taarifa zilizotolewa na serikali ya Misri kwa vyombo vya habari kwamba, harakati ya Ikhwanul Muslimin imeanzisha tawi la kijeshi kwa lengo la kupambana na polisi na jeshi la nchi  hiyo. Kiongozi huyo mwandamizi wa Ikhwanul Muslimiin amesisitiza kuwa, harakati hiyo itaendelea kupigania haki zake zote kwa njia za amani. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi karibuni kundi la watu waliobeba silaha lilishambulia kituo cha polisi  na kuwauwa  askari watano na wengine wawili kujeruhiwa. Serikali ya Misri ililifungamanisha shambulio hilo na kundi la Ikhwanul Muslimiin. Wakati huohuo, Mahakama moja nchini  Misri imetoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa watu 14 na wengine wanne kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma eti walishiriki katika shambulio dhidi ya kituo cha polisi nchini humo.

No comments:

Post a Comment