Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, February 11, 2014

Morocco inaamiliana vibaya na wahajiri wa Kiafrika


Morocco inaamiliana vibaya na wahajiri wa KiafrikaShirika la Kutetea Haki za Binadmu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya Morocco kuamiliana  kiubinadamu na wahajiri wa Kiafrika wanaopita nchini humo. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imeeleza kuwa, wahajiri wanaopita nchini Morocco wakitokea maeneo ya kusini mwa jangwa la Sahara na kuelekea barani Ulaya, wanakabiliwa na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kupigwa na kuwekwa rumande bila ya kufunguliwa mashtaka. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la HRW limeeleza kuwa, licha ya kufanyiwa marekebisho sheria za wahajiri na wakimbizi nchini humo, lakini bado vinaendelea kushuhudiwa vitendo visivyo vya kibinadamu vinavyofanywa na askari usalama  dhidi ya wahajiri.
Wimbi kubwa la wahajiri kutoka kusini mwa jangwa la Sahara limekuwa likipita nchini Morocco na kuelekea Uhispania, lakini limekuwa likikumbana na mateso wakati wa kuondoka nchini humo. Morocco inahesabiwa kuwa kivuko muhimu cha wafanya magendo ya dawa za kulevya na wahajiri haramu ambao hujaribu kuingia Ulaya kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment