Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, December 15, 2012

Wahadhiri wa kiislamu waaswa kufanya tafiti juu ya maisha ya Sheikh Abdullah Saleh Alfarsy

 Kadhi Mstaafu wa Kenya Sheikh,Hamad Kassim akitoa Historia ya Maisha ya Sheikh Abdalla Saleh Farsy katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh huyo aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960 kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.
 Mwanafunzi wa Sheikh Abdalla Saleh Farsy Sheikh Machano Hamadi Machano akitoa Historia ya Madarasa aliokuwa akifundisha Sheikh huyo na Masomo yake katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akitoa hotuba katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.
 
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk kulia akibadilishana Mawazo na Kadhi Mstaafu wa Kenya Sheikh,Hamad Kassim katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.
Baadhi ya Walimu wa Madrasa na Wanafunzi waliohudhuria katikaTamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960 kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SI MAI -MAELEZO ZANZIBAR.

Faki Mjaka- Maelezo
Wito umetolewa kwa Wahadhiri wa Kiislam Vyuo Vikuu na Madrasa nchini kufanya tafiti mbalimbali za maisha ya aliyekuwa Kadhi wa Zanzibar na Mfasiri wa kwanza wa Kuran kwa lugha ya Kiswahili Shekh Abadallah Farsy ili waweze kubuni njia mpya za kuamrisha matendo mema na kukataza maovu katika jamii.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk wakati alipokuwa akihutubia waumini wa Dini ya Kiislam katika Tamasha la kiislam la Zanzibar lililofanyika katika Jumba la Karsi ya Mfalme Forodhani Mjini Zanzibar.

Amesema Shekh Farsy alifanya mambo makubwa katika kuilingania jamii ya Afrika juu ya kumcha Mungu na kwamba jitihada zake zinapaswa kuthaminiwa kwa jamii kuendeleza harakati zake alizokuwa akizifanya katika uhai wake.
Waziri Mbarouk amesema Wahadhiri wa Dini ya Kiislam katika Vyuo na wale wa Madrasa wanapaswa kubeba jukumu hilo la ulinganiaji kwa kufanya tafiti mbalimbali na kubuni mikakati mipya ya kuilingania jamii katika kutenda mema na kukatazana mabaya yasiyompendeza Mungu.
Aliongeza kuwa Shekh Farsy aliwahi kuwa Kadhi wa Zanibar na Kadhi Mkuu Nchini Kenya na kujipatia umaarufu mkubwa katika kulingani na kutafsiri Quran kwa lugha ya Kiswahili.
Kwa upande wake Kadhi Mkuu Mstaafu wa Kenya Shekh Hamad Kassim wakati akielezea historia ya Shekh Farsy amesema elimu kubwa ya Dini aliyokuwa nayo Skekh huyo ndiyo iliyopelekea kuteuliwa kuwa Kadhi Mkuu nchini Kenya bila hata kuwa raia wa Kenya.
Ameeleza kuwa njia pekee iliyompelea kufanikiwa Kielimu ni kupenda kujifunza popote bila kuchoka kutoka kwa Mashekh tofauti ndani na nje ya nchi yake.
Naye Mkurugenzi wa Tamasha hilo la Kiislam la Zanzibar Jabir Khaidar amesema lengo la Tamasha hilo ni kujua historia za Mashekh wa Zanzibar ili jamii iweze kujifunza njia ambazo walitumia Mashekh hao katika kulingania jamii
Shekh Abadallah Farsy alizaliwa Unguja Februari 12,1912 na kufariki dunia Maskat Oman mwaka 1985 ambapo katika Maisha yake aliwahi kuwa Mfasiri wa Kwanza wa Kurani kwa lugha ya Kiswahili na Kadhi Mkuu wa Kenya kwa muda wa Miaka 10.

No comments:

Post a Comment