Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 17, 2012

Polisi yapinga uhusiano kati ya ANC na waliokamatwa


Polisi yapinga uhusiano kati ya ANC na waliokamatwa Polisi ya Afrika Kusini imetangaza leo kuwa imezuia njama ya kutaka kuuvamia mkutano wa chama tawala cha ANC iliyokuwa imepangwa na raia wanne wa nchi hiyo wenye misimamo mikali.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Rais Jacob Zuma na makumi ya maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Afrika Kusini. Wanaume hao wanne wenye umri kati ya miaka 40 hadi 50 walikamatwa jana Jumapili. Msemaji wa polisi ameeleza kuwa kuna ushahidi kwamba watu hao walikuwa wakipanga njama ya kutekeleza vitendo vya ugaidi katika maeneo mbalimbali ya Afrika Kusini na si katika mkutano wa ANC pekee unaoendelea kufanyika katika mji wa Bloemfontein huko katikati ya nchi hiyo.
Billy Jones msemaji wa polisi ya Bloemfontein amesema kuwa watu hao wametiwa mbaroni katika majimbo tofauti ya Afrika Kusini.
Keith Khoza msemaji wa chama cha ANC amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa wanaume hao wanne walikuwa wamepanga njama ya kuripua bomu kwenye hema kubwa kunapofanyika mkutano wa ANC ambapo Rais Zuma  na washiriki wengine wapatao 4500 wanakutana kwa siku ya tano ili kumchagua kiongozi mpya wa ANC katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

No comments:

Post a Comment